WANAFUNZI wa Chuo Kikuu
Kishiriki cha Mkwawa wamepanga kujitoa katika mchezo wa shirikisho la mpira wa
miguu ulioandaliwa na kudhaminiwa na kampuni ya vinywaji Grandmalt.
Akizungumza na mtandao
huu kwa njia ya simu leo, Waziri wa michezo katika serikali ya wanafunzi wa
chuo hicho Mlipano Henry alisema wila wamepanga kujitoa katika shirikisho hilo
endapo madai yao hayatasikilizwa na kutimizwa.
Amesema katika michuano
iliyofanyika mwaka jana walishiriki kwa mateso na kuahidiwa kutimiziwa kila
kitu mwishgoni kwa michuano jambo waliloachwa njiapanda na kampuni hiyo pasipo
maelezo ya kueleweka.
“Kwanza nasikitika sana
kuona tunatumiwa kama watoto na kampuni inayofanya biashara. Sisi ni watu
wazima ambao tunajua kuwa tunadanganywa. Mwaka jana kamapuni hii ilikuja
kutuomba kushirikia katika michuano hiyo bila kutupatia vifaa vya michezo na
kutuomba tutumie nguvu zeti ili mwishoni tupate kila kitu pamoja na kurudisha
gharama tulizotumia lakini baada ya michuano kuisha wakaona walichokuwa
wanatafuta wamekipata wakatuacha njiapanda wakisema hawana kitu” amesema Waziri
Mlipano.
Amesema waliahidiwa na kampuni
hiyo kuwa kila timu inayoshiriki itapewa jezi na mipira mitano mitano pamoja na
gharama zingine zilizotumika jambo ambalo hailikufanyika hadi leo.
“Nashangaa tena mwaka
huu wamekuja kwa njia ile ile wakitutaka tushiriki bila kutimiza ahadi za nyuma
hata kukumbishia tu. Pia waliahidi kuwa watakuja kupanda miti katika chuo chetu
kama sehemu ya utunzaji mazingira lakini hilo lilisahaulika siku ile ile
walipokuwa wakiahidi” amesema.
Hata hivyo amesema baada
ya kufanya nao mawasiliano na kuona hakuna kinachoendelea, waliomba kupewa
katoni 28 za vinywaji ili waweze kuuza na kununua vifaa walivyoahidiwa lakini
baada ya kuzungusha kwa muda mrefu waliambulia kupewa katoni 5 tu ambazo
haziwezi hata kukunua mpira.
“Sisi tunaamini kuwa ile
ni kampuni inayofanya biashara lakini kinachoonekana hapa wanataka kututumia
sisi kufanya biashara zao na mwishowe kutuacha kama wajinga fulani. Sisi tunasema
kuwa, kama ahadi za nyuma na madai yetu hatujatimiziwa hatuwezi kuingia mkenge
kama walivyotutumia mwaka jana. Haya siyo maamuzi yangu bali ni ya wachezaji
wenyewe” amesema.
Kwamba “hata kwa wale
wasiolielewa hili tunataka wajue ili wasije wakaingia mkenge kama sisi tulivyo
fanya mwaka jana” amesema.
Alipotafutwa kwa njia ya
simu kutolea maelezo juu ya jambo hilo, meneja wa kampuni ya Grandmalt na
mwandaaji wa mashindano hayo katika Mkoa wa Iringa Protas Singu amesema yeye
hakujua kama kuliwa na ahadi hizo ambazo wanachuo wanadai na kuahidi kukaa nao
mezani ili kumaliza tatizo.
“Nimepata malalamiko
hayo lakini kiukweli mimi binafsi sijui na kama yasengekuwa mashindano haya,
nisingejua kitu. Hivyo, nakuahidi kukupa mrejesho mara baada ya kukaa mezani na
kuyamaliza” amesema Singu.
Alipotakiwa kutolea
maelezo juu ya wanafunzi hao kutangaza kujitoa na huku ikiwa imebaki siku moja
tu ili mashindano yaanze, Singu alisema kila jambo linazungumzika na kufikia
mwafaka.
“Nisingependa tufikie hapo.
Tunaingia mezani ili tulijadili kwa pamoja na kushughulikia madai yote. Nina imani
kuwa tutafikia makubliano na hatimaye watashiriki” amesema.
Shirikisho hilo linatarajiwa
kuanza kutimua vumbi katika viwanja vya chuo kikuu cha Mkwawa jumapili ya Aprili
20 mwaka huu iwapo mwaka jana ilifanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu
Kishiriki cha Tumaini.

No comments:
Post a Comment