| Kushoto ni kijana ambaye jina halikutambuliwa mara moja akipigwa na polisi. |
| Kijana ambaye hana shati akichapwa na polisi aliye mbele yake. |
| Nyuma ya pikipiki ni jana anayeendelea kupigwa na polisi baada ya kuteguliwa mguu na kupasuliwa usoni huku mkono wake ukiwa umechubuka. |
Ni nje kidogo na stendi ya
daladala ziendazo Chuo cha Pipango na Nanenane ndani ya mji wa Dodoma, Polisi walipomkamata kijana
mmoja mbele yangu na kuanza kumpiga.
Wakati wanaendelea kumpa kichapo,
wananchi walitaka kujua kosa la huyo kijana ni nini ndipo alipojitokeza askari
mmoja na kusema ni mlevi.
Wakati hayo yakiendelea
nikashuhudia kwa macho yangu askati aliyekua amevaa mavazi ya kiraia akiwa na
boriti na kuanza kumpiga kijana huyo miguuni, mgongoni hata mikononi na
kumpasua usoni na kumtegua mguu.
Hali hiyo ilinisukuma kuchomoa
kamera katika mkoba wangu na kuanza kupoga picha kwa kiicho japo watu walikuwa
wengi iawa ni shida kupata picha lakini nilijitahidi kupata picha Fulani.
Nikaona haitoshi nikaamua
kumsogelea askari mmoja na kunza kumuuliza ni kosa gain kijana amelikosa kiasi
cha kuchapwa kama mnyama.
Wakati nikiuliza hivyo askari
huyo akwaita wenzake na kusema huyu ni mwandishi anatafuta nini hapa.
Kibao kilinigeukia nikaoneshwa
bunduki ndipo nilipofanikiwa kujichanganya na watu nikakimbia na ananchi
wasamaria wema wakaamua kunificha.
Zilisikika sauti za wananchi
wakisema “mlindeni mwandishi huyo ili akafikishe hayo kwa taifa zima ili watu
waone unyama wanaotufanyia polisi”.
Muda mfupi walitokea askari wa
kikosi cha kutuliza ghasia na kufukuza wananchi kwa kuwatishia bunduki jambo
lililowasononesha watu kuwa hawana uhuru.
“Akionekana mtu hapa tunamuwasha.
Ondokeni hapa mara moja hatuwataki hapa. Jitieni na kimbelembele chenu muone. Potea”
alisema askari.
Wakati hayo yakitendeka ikatokea
gari ya polisi na kumtupia yule kijana na kuondoka naye huku akiendelea kupigwa
kwenye ndani ya gari wakati anapelekwa kituoni.
No comments:
Post a Comment