masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, April 14, 2013

MWENYEKITI WA MTAA AWEKWA KIKAANGONI

Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa akiongea na wakazi wa mtaa wa Lukosi Kata ya Mkwawa Manispaa ya Iringa.


MWENYEKITI wa Mtaa wa Likosi Kataya Mkwawa katika Manispaa ya Iringa Kened Mahona (CCM) amekaangwa na wananchi mbele ya Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa kutokana na madai kuwa anatumia kuwaongoza.

Mahona aliingia kikaangoni jan baada ya wananchi kumsimamisha Mbunge alipokuwa anakwenda msibani baadaya mkutano uliopangwa kufanyika katika mtaa huo kuahirishwa baada ya msiba kutokea.

Wakimtaka Mbunge Msingwa kuwasaidia, walisema pamojana mkutano kuahirishwa wanamuomba awasilikilize japo kwa dakika chache kutokana na mateso na manyanyaso wanayoyapata kwa mwenyekiti huyo.

Kitoa malalamiko hayo, wananchi walisema mwenyekiti wao anatumia mabavu katika kazi yake hata kutumia madaraka yake kuuza ardhi ya wazi na pesa kuweka mfukoni mwake na kila anapotakiwa kutoleamaelezo anapanga mbinu za kuwabambika kesi wanaoonekana kuwa na nguvu ya kuhoji.

Wananchi hao wakiwa na jazba walisema wameamua kutoa malalamiko kwa Mbunge wao ili awasaidie vinginevyo itafikamahala mwenyekiti huyo atakula kichapo.

“Kuna mambo mengi hapa mtaani tumekuwa hatutendewihaki lakini mwenyekiti huyu tukimuuliza anakuwa mkali na kutuambia kuwa tuna fujo na kututishia kukamatwa kuwekwa ndani. Hivi huu nndioutaratibu wa uongozi? Tunakuomba Mbunge wetu utusaidie” alisema mwananchi mmojana kupigiwa makofi na wenzake.

Ilielezwa kuwa mwenyekiti huyo hajawahi kusoma mapato na matumizi na kila akiulizwa anakuwa mkali bila kutoa majibu huku ofisi akifungua akipenda.

“Imepita miaka mingi mapatona matumizi hatujawahi kusomewa. Tukitaka kuhoji, mwenyekiti ni mkali kama mbogo. Kama anabisha aseme hapahapa” alisema mwanachi mwingine.

Kwamba, “tunaeleza kwa masikitiko makubwa kwa sababu malalamiko yetu hata Mkurugenzi anayafahamu lakini hakuna utekelezaji. Tunajiuliza kuwa sisi ni miongoni  mwa wananchi walipa kodi au sisi ni wakimbizi? Tunachofanyiwa katika mtaa huu kinatufanya tujihoji mara nyingi bila kupata majibu. Tunakuomba Mbunge leo utusikilize kilio chetu” alisema.

Mbunge Msigwa alitumia kazi ya ziada kuwatuliza hasira kwanza wananchi hao kabla ya kumpa nafasi Mwenyekiti ili ajieleze na kujibu madai ya wananchi.

Alipotakiwa kujibu madai hayo Mwenyekiti Mahona alisema hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa mkutano umeahirishwa na kutaka utakapofanyika atakuwa na nafasi kubwa ya kutoa ufafanuzi.

Kutokana na mjibu hayo, wananchi walipandisha hasira na kutaka kutembeza kichpo mbele ya Mbunge jambo lililomfanya Msigwa kutumia busara kuwatuliza na kuwataka wawe na subira hadi watakapotangaziwa mkutano.

Wakati huo ofisa mtendaji wa mtaa huo Neema Kizwi aliyekuwa jirani, alilazimika kusimama mguu pande kuhofia kibano hicho kisije kikamgeukia.

Hata hivyo wanchi wamelalamika kuwa eneo la Chuo Kikuu cha Mkwawa limekuwa ni kijiwe cha vibaka ambao wanawatesa watu kwa kuwapiga nondo na kuwapora mali zao jambo ambalo Msigwa alisema linazungumzika na kutafutiwa ufumbuzi baada ya kujadili na uongozi wa chuo hicho.

Awali Mbunge Msigwa alikuwa afanye mkutano wa kiserikali katika viwanja vya  mtaa huo lakini ukaahirishwa baada ya kutokea msiba jirani na viwnja hivyo.

No comments:

Post a Comment