masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, April 6, 2013

UJENZI WA SOKO LA MTAA WA NGOME UTATA MTUPU


Jengo la vyoo vya soko jipya linaloendelea kujengwa katika mtaa wa Ngome Kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa linalodaiwa kujengwa kwa gharama ya shilingi 15 milioni.
 
WAKAZI wa Mtaa wa Ngome Kata ya Kihesa katika Manispaa ya Iringa, wamemtaka Mkurugenzi wa Manispaa kuunda tume ya wataalamu wa majengo ili kuchunguza uhalali wa ujenzi wa jengo la vyoo katika soko jipya linaloendelea kujengwa katika Mtaa huo.
 
Wakazi hao wameeleza kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na kutokuridhika na taarifa za gharama ya ujenzi wa jengo hilo na ukubwa wa jengo lenyewe.
 
Kwa nyakati tofauti wamesema kumekuwa na ubabaishaji wa ujenzi huo hali iliyosababisha hata mwenyekiti wa mtaa kutafutiwa makosa kwa kuwa amekuwa akisema ukweli.
 
Wameeleza kuwa lango la kutaka ufanyike uchunguzi ni kutaka kujua idadi ya bati zilizotumika, mifuko ya sementi mingapi, mawe kiasi gani, nondo kiasi gani na za aina gani, tripu ngapi za mchanga na tofati, misumari kiasi gani pamoja na mbao ngapi
 
“Siwezi kukubali hata kwa moto kuamini gharama za ujenzi huo. Kama gharama hizo ni za kweli, kwa nini ofisa mtendaji wakati anatoa taarifa alisoma barua ya kumsimamisha uenyekiti mwenyekiti wetu wa mtaa?” amesema mkazi mmoja.
 
Wamesema kila wakati wamekuwa na wasiwasi na taarifa alizokuwa akizitoa ofisa mtendaji wa mtaa huo kwa kile walichoeleza kuwa taarifa hizo zina utata muda wote.
 
“Huyu mtendaji wa mtaa huu hatumuelewi. Na ukifuatilia kwa umakini anashirikiana na watu wakubwa tu ili kupitia ujenzi wa soko hili kwa manufaa ya familia zao. Asifkiri kuwa watu wajinga. Tujua kila kinachoendelea lakini umefika muda wa kumwambia hatuna imani naye” amesema mkazi mwingine.
 
Mkazi mmoja anayeishi jirani na soko hilo ambaye ameomba jina lake lisiandikwe gazetini ameeleza kuwa mara kadhaa amewaona watu wakipita na sementi usiku na kuingiza kwenye nyumba moja ambaye jina tunalo.
 
“Mimi nimekuwa nikishuhudia semementi ikichukuliwa usiku kuanzia saa tano watu wakiwa wamelala. Utakuta watu wanachukua sementi na kuingiza kwenye nyumba moja hapa jirani. Wanafikiri wakituambia tu taarifa za ujenzi sisi ni wajinga tutakubali tu. Hizo ni kodi zetu tunazokamuliwa kila siku huku tukishindwa hata kununua chakula chetu tu. Bora ufanyike uchunguzi wa umakini tujue ukweli. Nakuhakikishia, ukifanyika uchunguzi wa uhakika haponi mtu hapa” kimesema chanzo chetu.
 
Machi 16, 2013 ofisa mtendaji wa mtaa huo Eliques Ngakonda akisoma taarifa ya ujenzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko hilo na kuhudhuliwa na watu 32 alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo la vyoo umegharimu 15 milioni bila kuainisha matumizi hayo jambo lililowafanya watu kuwa na miguno ya kila aina.
 
Sambamba na taarifa ya ujenzi ofisa huyo alisema hamtambui mwenyekiti wa mtaa huo Elizabeth Mkayula kama mwenyekiti kwa kuwa ameshaondolewa katika kiti hicho na kumkaimisha Prisca Mkusa hali iliyosababisha watu waliohudhuria katika mkutano huo kupinga vikali.
 
“Huyo tulimchagua sisi na tutamtoa sisi. Hatujamfukuza, huyo mnayemuweka wa kwenu. Mnamtoa mwenyekiti wetu kwani ninyi ni akina nani” zilisikika sauti hizo.
 
Hata hivyo utafiti uliofanyika umebaini kuwa kuenguliwa kwa mwenyekiti huyo ni ujenzi wa soko hilo kwa kuwa baadhi ya watu wanashindwa kuiba kwa kuwa mwenyekiti ni muazi na ni mkweli.
 
“Yapo mengi juu ya ofisa mtendaji huyo na wenzake anaoshirikiana nao lakini kilichokikubwa ufanyike uchunguzi wa ujenzi wa soko hilo kwanza” kimesema chanzo chetu.
 
Licha ya milioni 15 zinazosadikiwa kujenga vyoo hivyo, imeelezwa kuwa mashimo pekee yalijengwa kwa shilingi milioni 8 tofauti na zile 15 milioni zinazozungumziwa.
 
Mtu mmoja miongoni mwa wale wa kamati ya ujenzi ambaye ameomba jina lake lisiandikwe ameeleza kuwa kuna ujanja mkubwa umefanyika ambao ni wa machomacho.
 
“Zimekuwa zikitumika mbinu za ujanja. Kwa upande wangu siwezi kukubali na siwezi kusaini kuwa 15 milioni zimejenga jengo lile kwa sababu najua mbinu zilizotumika” amesema.
 
Mwenyekiti wa mtaa huo Elizabeth Mkayula alipotafutwa kutoa ufafanuzi zaidi alisema hawezi kusema chochote kwa kuwa hakushirikishwa.
 
“Siwezi kusema lolote kwa sababu ujenzi huo sikushirkishwa ila tu nilikuwa nikipigwa vita ili nisifuatilie kinachofanyika pamoja na kuwa mwenyekitu wa mtaa ndiye anayetakiwa kuwa mfuatiliaji wa karibu katika masuala kama hayo kwa sababu ndiye anayewajua watu wake na kuongea na watu wake juu ya maendeleo. Kwa kweli nisiwe muongo hapo sijui lolote” amesema Mkayula.


No comments:

Post a Comment