KUSHUKA
kwa kiwango cha ufaulu wa wanafaunzi nchini kumeelezwa kwamba ni dalili ya
jamii kushindwa kuwajibika katika elimu.
Haya
yamezungumzwa na Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya Tuwafikie Bovan
Mwakyambiki katika mahojiano maalum na mtandao huu leo.
Mwakyambiki
amesema ili mwanafunzi aweze kufanya vizuri ni lazima jamii inayomzunguka
iwe inafanya vizuri pia ambapo jamii ya watanzania kwa asilimia kubwa ni jamii
ambayo haijaipa sekta ya elimu umuhimu wa kutosha.
“Jamii
ya watanznia ni jamii ya watu ambao wapo bize kiasi cha kusahau kufuatilia hata
maendeleo ya watoto, ni jamii ya watu waliojengwa katika mfumo wa kujifunza
wakiwa shule na baada ya kumaliza shule hawaoni umuhimu wowote wa kuendelea
kujifunza na kujiendeleza” amesema Mwakyambiki.
Amesema
kila jamii ya watanzania ni jamii ya watu wasiopenda kujisomea na kuboresha
fikra zao na ni rahisi kumkuta mzazi ukipita zaidi ya mwaka mmoja bila kugusa
kitabu chochote ambacho kinaweza kumuongezea ujuzi katika mambo mbalimbali
“kila
mkoa niliopita, nje ya Dar es salaam ni vigumu sana kuyakuta maduka ya vitabu vya kijamii,
na mikoa mingine hakuna kabisa maduka ya vitabu vya kijamii. Hii ni dalili
kubwa sana kwamba
jamii yetu sio ya wasomaji, ni jamii ambayo inaona suala la elimu ni anasa.
Hakuna maendeleo yatakayoweza kupatikana kama
jamii haitaweza kubadilika. Wanafunzi ni watoto wetu, ni matunda ya jamii yetu.
Kama jamii ilivyobize kufanya mambo mengine na
kuona hakuna mda wa kuendelea kujifunza, vivyo hivyo hata kwa wanafunzi ambao
ni watoto wetu. Nao wanaona kuna mambo mengine ambayo wanapenda kuyafanya zaidi
ya kusoma kwa sababu hata wazazi nao wanatabia hizo” amesema.
Amesema
suala la kufeli kwa wanafunzi si la kuilaumu sekta moja bali ni jambo
linalotokana na mmomonyoko wa maadili kwa jamii nzima kwani kila jamii ina
wajibu wake.
“Watu
wengi wameshangazwa sana na matokeo ya kidato cha nne kwa wanafunzi waliofanya
mtihani wa taifa mwaka jana, jamii imekua ikilaumu sana serikari na wasimamizi
wa masuala ya elimu nchini na kusahau kuwa jamii bora hujengwa na jamii husika”
amesema.
Amesema
kufeli kwa wanafunzi ni urithi kutoka kwa wazazi na jamii inayowazunguka na
kwamba kila mti huzaa matunda ya aina yake, jamii ya watu wasiopenda elimu
huendelea kuambukiza tabia hizo hata kwa vizazi.
“Kufeli
kwa wanafunzi ni dalili ya kufeli kwa mzazi, kufeli kwa mwalimu, kufeli kwa
viongozi wa ngazi zote, ni kufeli kwa wasimamizi wa masuala ya elimu nchini,
kufeli kwa wanafunzi ni kufeli kwa jamii nzima. Kwa hali hii ninaamini kama tungeweza kutafuta kipimo cha kupima uelewa wa
Watanzania kwa mambo mbali mbali pia ninaamini kiwango cha kufeli kingekuwa ni
kikubwa kuliko hata hiki cha wanafunzi” amesema.
Ameitaka
jamii kubadilika na kujua ya kwamba, hakuna maendeleo yoyote kama hakutakua na
juhudi za msingi kuthamini na kuboresha utoaji na upokeaji wa elimu pamoja na
kuona uzito uliopo katika elimu na kutambua kutambua kwamba ni kioo na picha
yake halisi huonekana kwa uraisi kwa uzao wetu ambao ni wanafunzi.
“Ninapozungumzia
jamii ninagusa kila mmoja kwa nafasi yake, hata rais wa nchi
hii
yumo ndani ya jamii” amesema.
Ameongeza
kuwa jamii itakapochukua hatua ya kubadilika na kuthamini elimu pindi itakapojitambua na kujua wajibu wake
itawawawezesha vijana kuwatengeneza na kuwasimamia katika kuwaongoza na
kuwaonesha njia ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau wote wa masuala ya
elimu
“Kama
jamii itaweza kuwajibika na kujua kwamba ni wajibu wa kila mmoja wetu kuweza
kusimamia maendeleo ya elimu nchini, tutaweza kuwa na elimu bora na hakika
hatutaweza kuwapoteza wanafunzi kama ilivyo
sasa. Wanafunzi wengi
wanadharau elimu kwa kuwa hata wazazi au jamii wanaidharau pia. Mabadiliko ni
lazima yaanze na wewe, mimi mabadiliko ni sisi” amesema.
Ufaulu
wa wanafunzi wa kidato cha nne kwa mwaka 2012 umeshuka kwa 60% kulinganishwa na
mwaka 2011 walifeli kwa 46.4%, mwaka 2010 walikuwa 49.6%, mwaka 2009
walikuwa 27.5%, mwaka 2008 ilikuwa 16.3% na mwaka 2007 ilikuwa 9.7%.

No comments:
Post a Comment