masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, April 28, 2013

PADRE WA KANISA KATOLIKI AFA AJALINI






Hilo ni gari alilokuwa akisafiria Padre Alphonce Mhamilawa aliyefariki papohapo baada ya kupata ajali

JIMBO Katoliki la Iringa limempoteza Padre Alphonce Mhamilawa usiku wa kuamkia jana aliyekufa papo hapo kwa ajali ya gari.

Ajali hiyo ilitokea katika maeneo ya Changarawe Mafinga katika barabara ya Mafina – Makambako ambapo gari iliyosababisha ajali hiyo ilikimbia.

Kwa mujibu wa mashuhuda walisema kuwa katika maeneo hayo ajali nyingi zimekuwa zikitokea ambapo magari ya magogo yamekuwa ni chanzo.

Imeelezwa kuwa magari hayo yamekuwa yakifanya kazi usiku licha ya kuwa hayana taa jambo ambalo ni hatari kwa usalama barabarani.

Hata hivyo mashuhuda walieleza kuwa Padre Mhamilawa aligonga gari gilo kwa nyuma na kupoteza uhai paleple kutokana na gari lililokuwa limebeba magogo kutokuwa na taa au alama yoyote na mara baaba ya kusababish ajali hiyo kukimbia.

Licha ya gari hilo kukimbia halikuweza kutambuliwa haraka japokuwa gari alilokuwa akisafiria padre huyo lina namba za usajili T 434 APP.

Mpango wa mazishi unaendelea kufanyika ingawa marehemu anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Tosamaganga.

No comments:

Post a Comment