| Waimbaji wakiimba kanisani wakati wa Misa. |
| Jeneza la marehemu Padre Alphonce Mhamilawa likiwa kanisani Tosamaganga wakati wa Misa kabla ya kwenda kuzikwa. |
| Watu mbalimbali wakiusindikiza mwili makaburini kutoka kanisani. |
| Jeneza la marehemu Padre Alphonce mhamilawa likishushwa kaburini tayari kwa kuzikwa. |
| Mfunikio ukishushwa kufunika jeneza ndani ya kaburi. |
| Kitambaa chenye nembo ya chama cha kitume cha utume wa familia kikifunikwa juu ya mfuniko ndani ya kaburi kabla ya kufukiwa kwa udongo. |
| Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa jimbo la Iringa akiweka taji juu ya kaburi la marehemu Padre Alphonce Mhamilawa baada ya kuzikwa. |
| Mhashamu askofu Alfred Maluma wa jimbo la Njombe akiweka taji juu ya kaburi la marehemu Padre Alphonce Mhamilawa baada ya kuzikwa. |
| Mhashamu askofu Mkuu Norbert Mtega wa jimbo Kuu la Songea akiweka taji juu ya kaburi la marehemu Padre Alphonce Mhamilawa baada ya kuzikwa. |
| Mhashamu askofu mstaafu Emanuel Mapunda wa jimbo la Mbinga akiweka taji juu ya kaburi la marehemu Padre Alphonce Mhamilawa baada ya kuzikwa. |
| Kaka wa Marehemu akiweka shada kwenye kaburi. |
RAIS wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashau
Tarcisius Ngalalekumtwa amesema binadamu ana mahangaiko mengi yanayombabaisha
na kuchosha.
Ameyazungumza hayo alipokuwa akihubiri katika
Misa ya mazishi ya aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Ifunda Jimbo Katoliki la
Iringa Padre Alphonce Mhamilawa alifariki papohapo Aprili 26 mwaka huu kwa
ajali ya gari na kuzikwa katika makaburi ya Tosamaganga.
Alisema japokuwa binadamu anazongwa na matatizo
mbalimbali ambayo yanasababisha kupotea na kuvuruga mahusiano, binadamu
ametakiwa kuwa na uvumilivu.
“Maisha ya binadamu ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Tushiriki zawadi hiyo tukiwatendea wenzetu mema tukiyatimiza mapenzi ya Mungu”
alisema askofu Ngalalekumtwa.
Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa
jimbo la Iringa alisema binadamu anapasika kutumia nafasi aliyonayo hapa
duniani kwa ajili ya wengine hasa katika wakati mambo yanapobadilika na kuwa
kikwazo cha kumtafuta Mungu.
Hata hivyo alisema maisha ya mwanadamu yana
thamani kubwa japo kuwa mwanadamu amekuwa akiyachezea kwa mambo yake yasiyo na
msingi.
“Binadamu wanakata tamaa kwa sababu ya mambo
mengi ambayo chanzo chake ni binadamu mwenake au wenzake na kusababisha
mvurugano katika jamii” alisema.
Aliwataka binadamu hasa waamini wakristo kuwa
makini na baadhi ya watu wasio watakia mwma wengine ili waweze kujiepusha na
mvurugano unaoweza kujitokeza.
Amewataka wakristo kujenga utamaduni wa kuwa na
umoja hata pale ambapo wanakuwa katika mateso yanayowesa kusababisha
kuwasambaratisha.
“tujenge umoja na mshikamano. Mungu hapendi
tuhangaike bila sababu. Maisha ni mapambano, mapambano mengine hayana sababu.
Kila mtu awe ni chimbuko la maelewano. Ili
maisha yawe na mvuto, lazima binadamu awe na mapendo, umoja na mshikamno”
alisema.
Alisema marehemu Padre Mhamilawa atakumbukwa kwa
ushirikiano wake mkubwa aliokuwa nao na pia kwa huduma alizokuwa akizitoa kwa
watu mbalimbali za kiroho na kimwili.
Misa ya mazishi hayo iliongozwa na askofu wa
jimbo Katoliki la Njombe Mhashamu Alfred Maluma ambayo yalihudhuriwa na umati
wa watu kutoka ndani na nje ya jimbo ambapo maaskofu wanne walishiriki.
Maaskofu waliohudhuria katika mazishi hayo ni
Mhashamu askofu Alfred Maluma wa jimbo Katoliki la Njombe, askofu msaafu wa
jimbo la Mbinga Emanuel Mapunda, Mhashamu askofu Mkuu Norbert Mtega wa jimbo
Kuu la Songea na askofu wa jimbo la Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa
pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali.
Marehemu Padre Mhamilawa alizaliwa Julai 1, 1940
na kufariki kwa ajali ya gari April 26 katika barabara ya Mafinga – Makambako
katika maeneo ya Changarawe.
No comments:
Post a Comment