| Moja ya jengo la chuo cha kilimo kinachojengwa na asasi isiyo ya kiserikali kwa ajili ya kuwakomboa watu wa Kilolo |
| Miongoni mwa wananchi wa kijiji cha Ukwega Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa wanaonufaika na miradi ya asasi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na maendeleo ya watu wa Kilolo (MAWAKI) |
WAKULIMA viongozi wametakiwa
kuzingatia maelekezo na maagizo ya wataalamu ili waweze kuwa msaada kwa
wakulima wenzao kwa ajili ya kuresha kilimo chao.
Hayo yamezungumzwa na Daniel
Kalinga Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na maendeleo
ya watu wa Kilolo (MAWAKI) wakati wa mafunzo kwa wakulima viongozi
yanayofanyika katika ukumbi wa tabasamu Pomerini.
Kalinga ameeleza kuwa MAWAKI
imeamua kututoa mafunzo ka viongozi wakulima ili kuongeza uelewa wa wakulima vijijini
kwa ajili ya kuboresha kilimo kutokana na kuwa na uhaba wa wataalamu ambao
inakuwa ni vigumu kuwafikia wakulima wote.
Kalinga ambaye pia ni mratibu wa
mradi mpya wa kutegemeza uhakika wa chakula na maendeleo endelevu amesema
yanakwenda sambamba na utoaji elimu kwa wafugaji ili waweze kujikomboa kupitia
mifugo bora.
Ikiwa washiriki 30 kutoka vijiji
10 wanapata elimu hiyo kwa muda wa wiki moja, wakufunzi mbalimbali kutoka ndani
ya mkoa na nje ya mkoa wamepewa nafasi kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.
“Huu ni mwanzo tu wa mafunzo
ambapo tunajipanga kutoa mafunzo kwa watu wengi ili kuwawezesha wakulima wengi
kufikiwa na elimu kiurahisi bila kutegemea wataalamu pekee. Tumeona tukitumia
njia hii inaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kwa kuwa elimu ndogo inayotolewa
itawasaidia wengine” amesema Kalinga.
Washiriki hao wametoka katika
vijiji 10 vya Kata za Ukumbi, Mtitu, Ukwega na Kata ya Ng’uluwe (Pomerini).
Mbali na utoaji elimu kwa
wakulima na wafugaji, asasi hiyo inatoa huduma mbalimbali kwa jamii zikiwemo huduma
za afya, mazingira na ujasiriamali.
“Tumefanikiwa kujenga kituo cha
watoto yatima na wenye ulemavu, tumejenga bweni la wasichana kwa ajili ya
wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 Udzungwa, tumejenga bweni la wasichana shule ya
sekondari Lukani na Kitowo, katika sekondari ya Mawambala tumejenga vyumba 2
vya madarasa, Pomerini tumejenga mabweni ya asichana na wavulana chuo cha
ufundi na shule ya msingi Msengela imejengwa kwa nguvu ya wananchi kwa msaada
wa MAWAKI” amesema.
Amesema kwa mwaka huu wanasomesha
wanafunzi zaidi ya 82 japo kuwa idadi inaweza kuongezeka wakati wowote
kutokana na matokeo ya kidato cha 6 yanayotarajiwa kutoka muda mfupi ujao
pamoja na uhitaji wa wanafunzi wanaoendelea na masomo ya kidato cha kwanza.
Pia wananchi mbalimbali wananufaika
na mradi wa ufugaji nyuki ambapo MAWAKI inawawezesha vifaa mbalimbali vya
ufugaji.
No comments:
Post a Comment