masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, March 14, 2013

ASASI YA MAWAKI KUWAKOMBOA WANANCHI

Katikati ni katibu wa asasi ya MAWAKI Shemasi Paulo Boldrini akiwa na wahisani valontia kutoka Italia wakiwa nje ya chuo cha kilimo kinachojengwa na asasi hiyo katika shamba la Dabaga Seed Farm
ASASI isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na Maendeleo ya watu wa Kilolo (MAWAKI) imekusudia kuwakomboa wananchi waishio wilayani humo na maeneo jirani kwa kuwawezesha kielimu.

Uwezeshaji wa watu hao unatokana na miradi mbalimbali inayolenga kuleta maendeleo ya moja kwa moja hasa katika utaratibu wa utoaji elimu ya ujasiriamali na kilimo.

Asasi hiyo imeweza kubuni miradi mbalimbali ambayo inaifikia jamii kiurahisi kwa njia ya ushirikishaji wa pamoja na utoaji wa elimu bila gharama yoyote.

MAWAKI kwa hisani ya watu wa Italia imeanzisha chuo cha kilimo ambacho kinalenga kumkomboa mkulima kuboresha uzalishaji na kuongeza pato kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo bora.

Chuo ambacho hadi sasa inaendelea kujengwa, tayari madarasa manne yamekwisha kukamilika pamoja na bweni lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 80 huku majengo mengine ya madarasa, bweni lingine, ukumbi na bwalo la walimu na ofisi mbalimbali yakiendelea kujengwa.

Akiongea na mtandao huu, katibu wa asasi hiyo Shemasi Paulo Boldrini amesema chuo hicho kinajengwa kwa mkataba na serikali ili kuboresha kilimo katika utoaji elimu kwa watu mbalimbali.

“Tumeingia mkataba na serikali ili kujenga chuo cha kilimo kitakachotoa elimu katika ngazi ya cheti na diploma ili wakulima wetu waweze kujikomboa kiuchumi na waweze kuzalisha mazao mengi yatakayowasaidia kimaisha” alisema.

Kutokana na mkataba huo, serikali imetoa maeneo na majengo yanayotumika na shamba la uzalishaji wa mbengu cha Dabaga (Dabaga Seed Farm) ili kwa pamoja waweze kushirikiana katika uboreshaji na uzalishaji wa mbegu inayofaa kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kupata mbegu bora.

Naye kaimu meneja wa shamba hilo Lyimo Frank akiongea na mtandao huu ofisini kwake mesema kujengwa kwa chuo hicho kutaongeza tija na kuwapatia fulsa watu mbalimba kujipatia elimu na ujuzi katika kuboresha kilimo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara.

“Tunawashuru wenzetu MAWAKI kupata wazo la kujenga chuo kwa sababu kikijengwa chuo hapa kitakuwa mkombozi kwa wakulima ambao kila wakati wamekuwa wakilima na kuzalisha mazao machache tofauti na nguvu walizotumia. Hata uzalishaji wa mbegu utaongezeka kwa asilimia kubwa tofauti na ulivyo sasa kwa sababu hata wanafunzi wenyewe watakakuwa wanasoma kwa vitendo pamoja na kuwajibika katika uzalishaji” meisema Lyimo.

Amesema ili kufanikisha hilo, MAWAKI wamekwisha kupewa ekari 50 za ardhi ili wanafunzi watakapokuwa darasani waweze kujifunza na kufanya kazi kwa vitendo kupitia ardhi hiyo kwa kuzalisha mbegu unayostahili kwa uzalishaji.

Alitaja aina ya mbegu ambayo MAWAKI kupitia chuo watakuwa wanaizalisha kuwa ni Hybrid 6303 kwa kuwa ndiyo inayohitajika kwa wakulima wengi kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

“Dabaga Seed Farm” lilianzishwa wakati wa vita ya II ya dunia baada ya muingereza na mjerumani kupigana na mjerumani hushindwa ndipo Malkia Elizabeth alipomkabidhi kiongozi wa jeshi la uingereza Canal Ntown   hilo kwa ajili ya matumizi ya kufuga wanyama na kilimo.

Lengo la kumkabidhi shamba hilo Ntown ilikuwa kufuga ng’ombe wa maziwa na nyama ili nyama iweze kusafirishwa kwenda Uingereza pamoja na kulima zao la ngano kwa matumizi ya chakula.

Pamoja na kujengwa kwa chuo hicho, MAWAKI inashughulika na miradi mingi zikiwemo shule za chekekea, ujenzi wa zahanati na utoaji wa huduma za maji kwa jamii mbalimbali katika vijiji.

Kwa upande wa elimu, MAWAKI wanashule 6 za chekechea ambazo zipo katika vijiji mbalimbali vya Kitowo, Mtitu, Isuka, Lukani “A”, Lukani “B” na Ukwega.

Hata hivyo wanawasaidia wanafunzi katika kuendelea na masomo ya sekindari kwa kutenga fedha kila kijiji.

“Zaidi ya wanafunzi 300 wanasaidiwa katika kuendelea na masomo ya sekondari na hasa sana wale wasio na uwezo, watoto yatima na wale ambao wazazi wao wanaumwa” amesema Shemasi Paulo.

Ili kuwawezesha watu mbalimbali kiafya wanatoa huduma kwa wagonjwa ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi ambapo hadi sasa watu 100 wanapata chakula cha lishe na wengine kupata huduma mbalimbali za kiafya.

Sambamba na kuwasaidia waishio na virusi vya Ukimwi, wameanza kujenga zahanati ambazo zitakuwa zikitoa huduma za afya, kuwahudumia akina mama wajawazito na wale walishio na virusi vya Ukimwi ikiwa tayari zahanati ya Ukwega inatoa huduma.

Hata hivyo wana gari kwa ajili ya kuwasaidiawatu mbalimbali hasa wagonjwa katika vijiji mbalimbali ambapo muhitaji wa huduma huchangia mafuta kwa ajili ya kumuwezesha kukimbizwa katika matibabu.

Ushiriki wa mazingira ni jukumu la kila mmoja ambapo Mawaki kwa hushirikiana na shirika la Tulime lenye makao yake makuu Palemo (Italia) wamefanikiwa kupanda miti ekari 500 kwa ajili ya kuhifadhi mazingira.

Tangu mwaka 2002 shirika la Tulime limekuwa likishiri kikamilifu kwa kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kwamba ni jukumu la kila mmoja kuwajibika kutunza mazingira bila kushurutishwa.

Asasi ya MAWAKI ilianzishwa mwaka 2003 na kupata usajili mwaka 30 Januari 2004 na makao yake yapo kijiji cha Pomerini Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment