| Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu akimuangalia mgonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Mufindi |
| Mkuu wa Wilaya akiongea na baadhi ya wauguzi na wakunga |
| Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya Wilaya ya Mufundi katika maadhimisho ya siku miaka 60 ya uuguzi na ukunga. |
WATAALAMU wa kada
mbalimbali wakiwemo wa kutoka sekta ya afya inchini wametakiwa kutokutelekeza
taaluma zao na kuingia kwenye siasa na badala yake wawajibike katika nafasi zao
kwa ukamilifu, haki na usawa.
Haya yalizungunzwa na Mkuu
wa Wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya
uuguzi nchini.
Alisema wauguzi hawana
budi kutumia muda wao kwa ajili ya kuhudumia jamii katika uzalendo wa dhati kwa
kuwa bila wao huduma za afya haziwezi kwenda mbele sawia na mpango wa huduma
bora.
“Kazi yenu inahitaji
uvumilivu mkubwa kwa watu mnaowahudumia kutokana na mitazamo ya watu mbalimbali
juu yenu ila tu msikate tama kwani taaluma yenu ni ya pekee” alisema Kalalu.
Hata hivyo alisema
uuguzi ni taaluma ambayo haina ushindani kwa kuwa ni huduma inayohitji ujasiri,
kujitoa na usiri mkubwa.
“Tunajua kuwa huduma za
afya zina changamamoto nyingi kutokana na mazingira na watu wanaohudumiwa
ambazo zinakatisha tamaa na kumfanya muhudumu kuacha kazi au kutowajibila
lakini kazi yenu ambayo inabeba uhai wa watu msikate tama” alisema.
Kalalu amesema kazi ya
uuguzi inakwenda sambamba na haki na wajibu ambapo amewataka wauguzi kuwajibika
na kutenda haki kwa kutoa huduma bora bila kubagua.
“Lakini hata hivyo
lugha zetu hazijawa nzuri kwa wagonjwa japo kuwa si wote wenye lugha hizo.
Tujaribu kushauriana wenyewe kama watoa huduma na kusaidiana ili tusiwe vikwazo
kwa wateja wetu. Ukiwa na hasira huko ulikokuwa, usipende hasira yako
ukaimalizie kwenye sehemu yako ya kazi kwa sababu hao hawahusiki na jambo
lililokukasirisha” alisema.
Amesema kwamba pamoja
na mapungufu yaliyosemwa wauuguzi wasiwe sehemu ya mapungufu ya huduma aidha
kwa visingizio mbalimbali.
Hospitali ya Wilaya ya
Mufindi iliyopo katika mji mdogo wa Mafinga inakabiliwa na changamoto
mbalimbali zikiwemo za ukosefu wa vyumba maalumu vya kulaza wagonjwa, vitendea
kazi na uchafu mawodini na mazingira kwa ujumla.
Naye muuguzi mfawidhi
wa hospitali hiyo Stephen Haule akisoma taarifa kwa Mkuu wa Wilaya alisema
hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uchafu katika
mawodi ya wagonjwa na mazingira kwa ujumla kutokana na kukosa watu wa kufanya
usafi na kuomba kazi hiyo kupewa kampuni binafsi.
“Katika hospitali yetu
tunakabiliwa na chanamoto nyingi; kuna uhaba mkubwa wa vitendea kazi, kuna
uhaba wa majengo kwa ajili ya kuwalaza wagonjwa kwa mfano hakuna wodi pekee kwa
ajili ya majeruhi akinamama pamoja na upungufu wa rasilimali watu (watoa
huduma)” amesema Haule.
Kwamba mfumo wa maji
safi na maji taka pamoja na umeme haukidhi haja ya watumiaji kutokana na
kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha watumiaji tofauti na mwanzo ilipokuwa
ikitengenezwa.
Naye Mariam Jackson
mkazi wa jijini Dar es Salaam anayepta matibabu katika hospitali hiyo amesema
vyoo vya hospitali hiyo haviridhishi kutokana na kukosa maji ya kutosha na hata
kuzidiwa na uchafu ikiwa ni pamoja na uhaba wa dawa hali inayosababisha usumbufu
kwa wagonjwa.
Kwa upande wake muuguzi
msaidizi wa huduma za macho ambaye pia ni msaidizi wa muuguzi Mkuu wa Wilaya
Michael Sanga alisema wanakabiliwa na uhaba wa wauguzi ambapo wauguzi waliopo
wanalazimika kufanya kazi kupita kiwango ndiyo sababu ya kuwa na majibu ambayo
si mazuri kwa wagonjwa.
Hospitali ya Wilaya ya
Mufindi ina vitanda 170, wauguzi 214 ambapo kwa siku akina mama wanojifungu ni
kati ya 20 hadi 32 na inahudumia watu zaidi ya 300,344.
Baraza la uuguzi na
ukunga Tanzania lilianzishwa 19 Machi, 1953 ambalo zaidi ya 60% ya wanataaluma
wote katika sekta ya afya ni wauguzi na wakunga.
No comments:
Post a Comment