| Mapadre wakimwa kwenye maandamano kuingia kanisani kwenye Misa ya kubariki mafuta nyuma ni Mhashamu askofu Tarsisius Ngalalekumtwa wa Jimbo la Iringa. |
MAKUHANI wa Kanisa wametakiwa waaminifu na kuridhika
na utii kwa kuwa wapole wenye unyenyekevu na na kutokuruhusu tamaa kuwaingia na
kufanya kazi kwa busara katika kuwahudumia wanadamukatika safari ya kuutafuta
wokovu.
Haya yamezungumzwa leo na askofu wa Jimbo Katoliki
la Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa alipokuwa akihubiri katika Misa ya
kubariki mafuta iliyofanyika leo katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Parokia ya
Kihesa.
Askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni Rais wa Baraza la
Maaskofu Tanzania amesema kuhani anayefanya kazi kwa haki na uaminifu kwa
kuwatumikia wanadamu bila ubaguzi kwa kuwatakatifuza anawafanya kuwa safi ili
kuwawezesha kuufika utakatifu naye kwa kuwafanya hivyo atakuwa mtu wa Mungu
aliyekamilika.
“Tunajijua kuwa sisi ni wadhaifu, tunaathirika na
hewa chafu ya ulimwengu, tunaishi katika ulimwengu uliojaa kila aina ya uchafu,
ninyi msio na daraja lolote la kipadre tunahitaji maombi yenu. Endeeleni kutulea,
kutulinda ili mwovu ibilisi asije akaendelea kutunajisi na kutupotosha. Mtuombee
ili tuweze kuwalea ninyi ndugu zetu ili tuwe na upendo usio na unafiki. Tuoombeeni
ili kuwafanya ninyi kuwa ni vyombo huru katika utumishi na kumtafuta Mungu kwa
bidii” amesema askofu Ngalalekumtwa.
Amesema makuhani ni daraja la kuwawezesha wanadamu
kuufikia utakatifu wa Mungu ambapo wanatakiwa kuheshimiwa na kuvikwa mavazi ya
pekee yanayolinda heshima na busara yake ili waweze kutenda mema daima.
“Makuhani wanatakiwa kuwa washauri wa kiroho kwa
wanadamu wenzao ili wawawezeshe kuyafikia makusudio ya Mungu. Watakapokujikubali
na kutenda yale ambayo Mungu anayataka, ndipo watakapokuwa watu wa Mungu. Wanapasika
kuukumbatia msalaba, Injili toba hizo ndizo silaha za kupambana na mwovu
ibilisi” amesema.
Amesema kuwa Makuhani wakumbuke kuwa kazi yao ni
kuendeleza kazi yake Kristo ya kuwaokoa wanadamu na kwamba Yesu Kristo lazima
habari zake zitazungumziwa wakati wote ulimwenguni.
“Mwaka huu wa Imani uwe ni mwaka ambao kwenu ni wa
kutuombea sisi ili tusilegee katika utumishi wetu ili hamu yetu na kazi zetu
kwenu zisirudi nyuma bali tuwe na bidii ya kumtumikia Mungu na kumkumbatia bila
kuchoka; tujaliwe kuwa walimu wa Sala kwenu, tuadhimishe liturujia kwa nidhamu,
tusiwe waigizaji wa kutenda, kujitoe kwa imani na upendo kwenu” alisema.
No comments:
Post a Comment