| Mkuu wa wa Mkoa wa Iringa Christine Ishengoma akiweka jiwe ya msingi katika chanzo cha maji cha Mawelewele. |
| Kikundi cha sanaa cha Mkwawa magic site kikifanya maagizo katikauwanja wa mkutano yalipofanyikia maadhimisho ya wiki ya maji kijiji cha Mkoga. |
| Mkuu wa Mkoa wakiwahutubia wananchi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kijiji cha Mkoga. |
MKUU wa Mkoa wa Iringa Christine
Ishengoma amewataka mamlaka ya maji Iringa (IRUASA) wasiwabambikie wananchi
bili za maji huku wakitaka kuwa makini na kutoa bili za uhalali kulingana na
matumizi ya mtumiaji.
Ishengoma ameyasema hayo katika
kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji yaliyofanyika katika kimkoa katika
kijiji cha Mkoga katika Manispaa ya Iringa.
Amesema kumekuwa na malalamiko ya
mara kwa mara juu ya ankara za maji yakidai kuwa
bili zinazotolewa na idara ya maji si sahihi na kuwataka wananchi ambao wanaona
bili zao sipo tofauti wasiogope kuwaeleza wahusika ili waweze kulimaliza tatizo
hilo badala ya
kubaki wakilalamika bila kutoa taarifa.
Kabla ya maadhimisho hayo
Ishengoma alikwenda kukagua chanzo cha maji cha Mawelewele pamoja na kuweka
jiwe la msingi katika chanzo hicho, akafika kukagua tanki la maji Kitasengwa na
baadaye kukagua mradi wa ujenzi wa vyoo katika shule ya msingi Mkoga sambamba
na kuwahutubia wananchi kijijini hapo.
Ishengoma amewataka wananchi
kutunza vyanzo vya maji na miundombinu sambamba na kutoa ushirikiano na
wataalamu wa maji ili maji yatakayozalishwa yawe safi na salama kwa afya ya binadamu.
“Mradi huu si wa serikali bali ni
wenu wananchi. Kwa hiyo, ninawaomba muutunze na kuulinda ili maji yaweze kudumu
na kutumika kwa watu wote. Msiharibu miuundombinu wana kuchafua na kuharibu
vyanzo vya maji” alisema Ishengoma.
Amesema endapo kila mtu
atawajibika ipasavyo katika sehemu yake katika suala ya maji, kila mwananchi
atapata maji safi
na salama kwa gharama nafuu.
Awali injinia wa maji Shaban
Jellan ambaye pia ni katibu tawala msaidizi sehemu ya maji akisoma taarifa ya
mradi huo alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uharibifu
wa vyanzo vya maji hali inayosababisha maji kupungua na wakati mwingine
kupatikana machafu.
Mradi huo hadi kukamilika jumla
ya shilingi 427,462,110 zinatarajiwa kutumika ambapo wananchi wanaotarajiwa
kunufaika ni wakazi wa Mawelewele, Kitasengwa na Mkoga ikiwa wananchi
wanatakiwa kuchangia shilingi 9,530,302.75 sawa na asilimia 2.5 huku serikali
Kuu ikitoa shilingi 371,681,807.25 sawa na asilimia 97.5.
Amesema kufikia Aprili 27, 2013
mradi unatarajiwa kuwa uwe umekamilika ambapo hadi sasa wananchi pekee wamekwisha
kuchangia shilingi 7,600,000/= kwa ajili ya ujenzi huo.
Mradi ulianza kutekelezwa Januari
28, 2013 kwa muda wa miezi 5 ambao unatarajia kunufaisha wananchi zaidi ya 2392
kwa umbali wa mita 400 kutoka kwenye makazi ya watu.
No comments:
Post a Comment