masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, March 24, 2013

WAKRISTO WAADHIMISHA SIKU KUU YA MATAWI

Baadhi ya Wakristo wakatoliki wakiwa na matawi ya mizeituni kufunya kumbukumbu ya kumpokea mwokozi wao kama walivyofanya wana wa Yerusalemu.

Waamini wakiwa na matawi mbele ya jukwa la Kichangani wakisubiri Padre ayabariki ili kuanza maandamano kuelekea kanisani.


Waamini wakiwa kwenye maandamamo yaliyoanzia Kichangani kuelekea Kanisa Kuu la Kiaskofu Kihesa.

Wanakwaya wa Kwaya ya Mt. Cecilia Parokia ya Kihesa wakiwa kwenye maandamamo kuingia Kanisani.
USALITI wa kisiasa umetajwa kuwa ni chanzo cha unyonyaji na dhuruma ya haki za wengine.

Haya yamezungumzwa na Padre Ponsiano Myinga wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu iliyofanyika leo katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Parokia ya Kihesa.

Amesema usaliti umezaa udanganyifu na upotoshaji wa mambo ya wazi na kusababisha mitafaruku ya isiyo ya lazima.

Amesema usaliti unatokana na watu kutumia rushwa katika kuhadaa haki za wananchi wasio na sauti.

Amemtaka kila mmoja kutimiza wajibu katika nafasi yake kwa kutenda haki na usawa ili mwingine asiumie au kuumizwa kwa ajili yake.

Aidha amesema kutokutimiza wajibu kwa uaminifu ni kumsaliti Kristo.

Wakristo nchini wanaungana na wakristo wote duniani kufanya kumbukumbu ya kumpokea Yesu Kristo akitokea Caprenaum kwenda Yerusalem wakiwa na matawi ya mizeituni wakimshangilia na kumlaki.

No comments:

Post a Comment