masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, March 28, 2013

HALI YA CHAKULA MBAYA

Mratibu wa baraza la vijana chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akitoa maelezo wakati alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hizi juu ya hali ya vijiji kupoteza matumaini ya mavuno kutokana na kuuziwa mbegu feki.

HALI ya chakula katika vijiji vya Magulilwa, Nega “B” na Ndiwili vilivyopo Kata ya Magulilwa katika Wilaya ya Iringa, hali ya chakula hairidhishi kutoka na kupata hasara katika mazao waliyopanda.

Katika nyakati tofauti imeelezwa kuwa hali ya chakula inaonekana kuwa tete kutokana na mbegu walizozipanda kuwa kuonekana kuwa zilikuwa feki.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo Hanifa Mgata mkazi wa kijiji cha Magulilwa alisema hali ya chakula katika kijiji hicho inatia wasiwasi kutokana na mazao yao kutokuchanua inavyostahili na kuendelea kuduma licha ya kupandia na kukuzia mbolea.

“Tumejitahidi sana kulima kwa kutumia mbolea pamoja na kutunza mashamba yetu lakini hali inayoonekana haituridhishi. Mahindi yanadumaa lakini baadaye tumeambiwa kuwa mbegu tulizozipanda hazikuwa halali” alisema Mgata.

Alisema licha ya kuwa na wataalam wa kilimo ambao walikuwa wakitoa maelekezo kwa wakulima, matokeo yamekuwa tofauti na matarajio yao licha ya kuwa wametumia nguvu nyingi na gharama kubwa katika uundaaji mashamba, ulimaji na utunzaji kwa ujumla.

Kwa upande wake Hadson Mvena alisema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya chakula inayotokana na hali mbaya ya mazao ya chakula.

“Tuna hali mbaya ya chakula pamoja na kuwa tulilima. Changamoto hii inatokana na kuuziwa mbegu mbaya ambayo haijatusaidia. Hatui la kufanya kwa sababu kama ni maji yamekwisha kumwagika na hatuwezi kuyazoa. Kwa upande mwingine unawalaumu sana wataalam wetu wa kilimo kwa kuwa hawakuwa msaada kwetu hata pale walipoona tunanunua mbegu isiyofaa na kutuacha huku wakijua kuwa sisi tunawategemea wao kitaalam” alisema Mvena.

Alisema haina maana ya kuwepo wataalam wa kilimo wasio msaada kwa wakulima ambao kwa makusudi wanapoona tatizo hawatoi ushauri.

Katika hatua nyingine mratibu wa baraza la vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (BAVICHA) Iringa Aidan Salehe amesema tatizo la mazao linalojitokeza katika vijiji hivyo ni matokeo ya kuwa na viongozi wasio na mipango mizuri ya kuwasaidia wananchi.

“Tulitarajia uwepo wa viongozi yaani mbunge na mwenyekiti wa halmashauri, watakuwa na mipango mizuri kwa watu wao ambao ni wakulima lakini kumbe ni sawa na tu na watu wangeishi bila kuwepo na viongozi” alisema.

Alisema matatizo hayo yanatokana na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM) kupuuza kilimo katika nchilicha ya kuwepo na kaulimbiu ya kilimo kwanza na kwamba mapendekezo yao kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa aunde tume ya uchunguzi kuhusiana na tatizo hilo.

“BAVICHA tumemshauri Mkurugenzi amfukuze ofisa kilimo wa halmashauri kwa kushindwa kutoa maelekezo ya kitaalamu kwa wakulima kinyume na wajibu wake unaomtaka asimamie kilimo muda wote na hata mabwana na mabibi shamba wa kata nao wafukuzwe ili kuleta dhana ya uwajibikaji” alisema.

Licha ya kuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga William Mgimwa (CCM) kuwa mjumbe wa kamati ya kilimo, maliasili na mazingira amelalamikiwa kutokuwa makini kwa kutoa mkazo kwa watumishi wa kilimo wanaobeba dhamana ya uwajibikaji kwa wakulima.

“Kwa kuwa CCM imeshindwa kusisitiza watumishi wote kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chma chama chao kwa vitendo ambapo mbunge Mgimwa ndiye msimamizi wa ilani hiyo akatika maeneo yaliyoathirika, tafsiri yake ni kwamba ameshindwa yeye na CCM yake kwa mujibu wa ilani yao Ibara ya 33 kifungu kidogo B” alisema.

Mmoja wa wataalam wa kilimo katika Kata ya Magulilwa alipoulizwa juu ya tatizo hilo alikiri kulifahamu na kwamba hayo ni matokeo ya kupokea maagizo ya utekelezaji na kufunga nafasi ya kutoa ushauri wa kitaalam.

Mtaalam huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini alisema kuwa mbegu hiyo waligundua kuwa siyo nzuri lakini walipojaribu kutoa ushauri waliambiwa kuwa hayo ni maagizo siyo mjadala.

“Tuliiona ile mbegu habridi namba 614 kuwa ni feki lakini tulipojaribu kutoa ushauri wa kitaalam kuwa ibadilishe, tuliambiwa kuwa serikali imeshapanga kwa hiyo kilichobaikia ni utekelezaji tu ndiyo maana tuliamua kukaa kimya kwa sababu tumepewa maelekezo ya kiutendaji” kilisema chanzo chetu.

No comments:

Post a Comment