masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, March 28, 2013

MATUMIZI MABAYA YA MUDA NI CHANZO CHA WANAFUNZI KUFELI

Baadhi ya wanafunzi wakimsikilza mwalimu kwa umakini wakati wa semina.

Mwalimu Nyaulingo Yustino akitoa maelekezo ubaoni kwa wanafunzi wakati wa seina.
MATUMIZI mabaya ya muda yametajwa kuni ni sababu ya wanafunzi kufeli mitihani kutokana na kutokuwa na ratiba nzuri zenye malengo kwa ajili ya kujisomea.

haya yamezungumzwa na mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Mgololo Nyaulingo Yustino alipokuwa akitoa semina kwa wanafunzi wa (T.Y.C.S) iliyofanyika kikanda katika ukumbi wa Parokia ya Mgololo.

Amesema muda mwingi wanafunzi waliowengi wamekuwa wakifanya mambo yao na kutokuzingatia masuala ya kujisomea hali inayosababisha wakati wa mitihani kufanya vibaya na kuwalaamu walimu pasipo sababu.

"Wanafunzi wengi hawajui matumizi ya muda. Muda mwingi wanatumia katika facebook, simu za viganjani na kuangalia video visivyo na maana. Hali hii inawajenga kuwa watu wa mitandao badala ya uwa watu walioelimika" amesema Nyaulingo.

Hali hiyo imesababisha wanafunzi wengi kujiingiza katika mapenzi na kusahau mambo ya muhimu wanayotakiwa kuyafanya na kuwajibika kama wanafunzi wawapo darasani au wawapo majumbi wakati wa mapumziko.

"Utashangaa wanafunzi wanashinda kwenye nyumba za starehe badala ya kuutumia muda huo katika kusoma na kuomba msaada wa kimasomo kwa pale wanaposhindwa" amesema.

Akitoa maoni yake kwa wanafunzi, Haluni Mnoga mwanafunzi wa shule ya sekondari Mgololo amesema chanzo cha wananfunzi kutokutumia muda vizuri ni mmomonyoko wa maadili uliokithiri ambapo mwanafunzi anathamini mambo ya anasa na kuacha mambo yatakayomsaidia maishani mwake.

"Wanafunzi tumejisahau sana kuwa tunapaswa kuwajibika katika nafasi zetu ili kuweze kuandaa maisha yetu hapo baadaye. Ila tatizo ni mmomonyoko wa maadili kwa vijana" amesema.

Amesema ili wanafunzi waweze kufahamu nini wanatakiwa kukifanya, wazazi na walezi wanapaswa kushirikiana na waalimu ili kuwajenga watoto katika maadili yanayostahili badala ya wazazi na walezi kuwaachia waalimu pekee malezi.

Jenifa Massawe mwnafunzi wa shule ya sekondari ya Mgololo amesema makundi ni chanzo kikubwa cha wanafunzi kujisahau na kufanya mambo wasiostahili.

"Wanafunzi wengi tunaangamia kwa sababu ya makundi tunayokutana nayo shuleni na mitaani. Imefika wakati wanafunzi hatuwasikilizi hata wazazi au walezi wetu kwa sababu tayari tunajivunia makundi yasiyo na maana. Kikubwa zaidi ili tufanikiwe katka masomo yetu ni kuwa watii, wasikivu na kujishughulisha na mambo ya kiroho" amesema Massawe.

Hata hivyo imeelezwa kuwa hata wazazi nao ni chanzo cha wanafunzi kufanya vibaya kwa kuwa wapo baadhi ya wazazi wasioelewa maana ya elimu na kuwafanya watoto wao kama watumwa jambo linalowasababisha kutopata muda wa kujisomea.

"Hata wazazi wetu wengine ni chanzo cha sisi kufanya vibaya. Wanafanya watoto wao kama watumwa, wanawapatia kazi nyingi huku wakijua kuwa mtoto au watoto wanasoma na mtoto akichoka hawezi kusoma tena" amesema.

No comments:

Post a Comment