| Joseph Mungai akifafanua zaidi barua yake aliyoiandika kwa tume ya kuchunguza anguko la elimu kwa mwaka 2012 kwa waandishi wa habari. |
| Joseph Mungai akijibu swali aliloulizwa na Katibu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Iringa (IPC) Francis Godwin (kulia). |
| Joseph Mungai akiwashukuru waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo naye. |
WAZIRI wa zamani wa elimu
Joseph Mungai, ameipa somo Tume ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda iliyoundwa kwa
ajili ya kuchunguza matokeo mabaya kuliko yote ya mitihani ya kidato cha nne yaliyowahi
kutokea hapa nchini, akiitaka kuzitolea
uvivu taasisi mbili za umma ambazo ni Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na
Taasisi ya Elimu nchini (TIE).
Mungai
aliyeiongoza Wizara ya Elimu wakati wa serikali ya awamu ya tatu mwaka
2000-2005 sambamba na kuwa Mbunge wa Mufindi Kaskazini,amesema inafaa matokeo
ya mitihani yawe yanatangazwa kwa uwazi hata kama
ni mabaya tofauti na ilivyo sasa.
Katika
barua yake ya wazi ya Machi 29 mwaka huu yenye kumbukumbu namba
JJM/2013/ELIMU/19 iliyoandikwa kwenda kwa Mwenyekiti wa Tume ya Elimu
iliyoundwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wa
kidato cha nne mwaka 2012,
Mungai
ameitaka tume hiyo irejee utafiti uliofanywa na Wizara ya Elimu na Ofisi ya
Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mwaka 2010 ambayo
ilifanya utafiti kudadidi sababu za ufaulu mbaya ambayo pia serikali ilishindwa
kuusoma bungeni.
Katika
barua yake kwa tume hiyo, Mungai anahoji kwa nini ukweli ulifichwa licha ya
taarifa hiyo ya utafiti kuwapo kwenye
maktaba za Wizara na kwamba anayoyasema hivi sasa ameyapata kutoka taarifa moja
isiyo ya siri ndani ya Wizara ya Elimu.
Hata
hivyo, Mungai ameitaka tume hiyo ieleze wazi wazi kwamba Taasisi ya Elimu (TIE)
iagizwe na iachiwe kutekeleza wajibu wake wa kisheria chini ya sheria ya elimu
ya mwaka 1995 ya kuandaa na kuboresha mitaala.
“Tume
ya Waziri Mkuu (Pinda) ifanye kwanza rejea ya maandiko ya Wizara ya Elimu
ambayo ni Nyaraka za Elimu za mwaka 1999 hadi 2005 na Sheria ndogo za Elimu au
kanuni za elimu zilizotungwa kuyapa maboresho hayo uzito wa kisheria
yamepelekwa nyaraka za kale kabla ya wakati wake…Hii itasaidia badala ya
kutumia muda mwingi na fedha nyingi kugundua upya gurudumu,” inasema sehemu ya
barua hiyo ya wazi kwenda kwa Tume ya Waziri Mkuu.
MITAALA YA ELIMU
IPO
Waziri
huyo wa zamani wa Elimu amemkejeli pia
Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia kuhusu kauli yake aliyoitoa Bungeni
miezi michache iliyopita kwamba nchi inaongozwa bila mitaala ya elimu kwamba
haina ukweli kwa kuwa mitaala hiyo ipo isipokuwa kuna ‘madudu’ katika taasisi
za umma zinazohusina na elimu.
Alisema
Mbatia aliitoa kauli yake bungeni pasipo kufanya utafiti wa kina na kwamba hata
wapinzani wa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wanajua kwamba wanasiasa
huamua bila kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri wa kitaaluma kuhusu elimu ya
taifa letu.
“Kwa
hiyo mimi ninaimbia tume ya Waziri Mkuu kwamba utaratibu sahihi wa kupanda
madarasa kwa kufaulu uliowekwa na Waraka wa Elimu namba moja na namba mbili wa
mwaka 2002 urejeshwe na uimarishwebila kuchelewa ambayo mwalimu mkuu siku zote
anayo madaraka ya kukaririsha kama mwanafunzi hajazijua zile ‘K’ 3 yaani
kusoma,kuandika na kuhesabu,”Alisema Mungai.
=========================================
Joseph
J.Mungai MB (mstf0
P.O.BOX
34 Mafinga
S: 0753 192999 BP: jjmungai@tatepa.com
BARUA
YA WAZI KWA TUME YA ELIMU
YA
KUFELI 60% MTIHANI WA KVI 12012
ILIYOTEULIWA
NA MHE WAZIRI MKUU
29/03/2013
Kumb Na. JJM/2013/ELIMU/19
Kwa Mwenyekiti
Tume ya Elimu ya Kufeli KIV
Ofisi ya Waziri Mkuu
DAR ES SALAAM
Ndugu Mwenyekiti
KUONGEZEKA WANAOFELI KIV KUTOKA 9.7%
MWKA 2007 HADI 60% 2012
1.1
Nnawapongeza kwa kuteuliwa na ahsante kutupa fursa wadau fwa elimu kuwaletea
maoni na au/ushauri.
2.0
Mimi ni mdau wa elimu, niliyewahi kuwa Mwenyekiti mwanzilishi wa Mufindi
Education Trust (MET) iliyoanzisha katika wilaya ya
Mufindi na kuziendesha kwa
mika zaidi ya 10
Sekondari 9 za: (1) JJ Mungai (2) Sadani ( 3) Itengule ( 4) Igowole
( 5) Itandula ( 6) Mgololo ( 7 ) Kibengu ( 8) Mdabulo na ( 9) Nyololo; ambazo
sasa ni za serikali. Aidha nimewahi kuwa waziri wa Elimu na Utamaduni
mwaka 2000 hadi 2005.
3.0 Kabla ya kutoa ushauri naoba
kuipa Tume yako ufahamu wa ukweli ufuatao:
3.1
Kufeli mwaka 2012 kidato cha Nne (KIV) kwa asilimia 60 halikuwa tukio
lililoibuka ghafla bali waliofeli ( Division 0) mtihani huo waliongezeka kutoka
mwaka 2007:9.7% ; 2008:16.3%; 2009:27.5%; 2010:49.6%; 2011:46.4% na sasa
2012:60%!!!!!
3.2
Kabla ya hapo waliofeli kidato cha Nne (KIV) WALIPUNGUA kutoak mawka
1998:24:3%:; 1999:20.0% 2000:21.6% 2001:22.6%, 2002:12.7%; 2003:12.2%,
2004:8.7%, 2005:10.7%, 2006:10.9%, na 2007:9.7% wastani wa kufeli 2004 hadi
2007 ni 10%. Tazama hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Utamaduni ya mwaka
2005/2006 kielelezo Na. 75.4 ukurasa wa 100; na BEST ( Basic Statics in
Education, National Data) ya miaka husika.
3.3
Kati ya 2004 na 2007 waliofeli kidato cha Nne walikuwa wastani wa 10%
ambayo inavumilika. Kwa nini kati ya 2007 na 2008 kulikuwa na mruko
kutoka 9.7% hadi 16.3%? Huo ukawa ndio mwanzo wa kuonge zeka
kila mwaka hadi kufikia
60% ya mwaka huu!!!!! Wizara ya Elimu na
OWM-TAMISEMI baada ya matokeo mabaya ya mwaka 2010
walifanya “utafiti kudadisi sababu za ufaulu huo mbaya” na
taarifa yake ipo kwenye maktaba a Wizara” na iliandaliwa kauli ya waziri isomwe
Bungeni”, lakini hadi leo haikusomwa. Ukweli ulifichwa; na
mficha ugonjwa kifo kitamuumbua. Nukuu zangu kutoka Taarifa
moja isiyo ya siri ya
ndani ya wizara ya Elimu.
4.0
Kwa maoni yangu maboresho ya Elimu ya Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo
yanaweza kusomwa katika maandiko mawili ya
Wizara ya Elimu yaitwayo: (a) Nyaraka za
Elimu 1999 hadi 2005, na ( b) Sheria ndogo za Elimu au kanuni za Elimu
zilizotungwa kuyapa maboresho hayo uzito w akisheria yamepelekwa
NYARAKA ZA KALE (ACHIVES) kabla ya wakati wake. Maboresho yamewekwa kando
moja baada ya jingine au hayakusimamiwa
ipasavyo na Elimu yetu imerudi ilivyokuwa kabla ya mwaka 2000.
USHAURI:
5.0 Kwa kuwa Elimu ni nyenzo
muhimu sana kuliko zote katika kuboresha nguvu kazi ya Taifa na
kucho cchea maendeleo ya nchi nimeamua kutonyamaza na kuwa muwazi
kabisa, ingawaje mimi ni mwanasiasa niliyestaafu. Kwa hiyo NASHAURI mambo
yafuatayo:
5.1 Utaratibu sahihi wa
kupanda madarasa kwa ufaulu ( achievement based progression) uliowekwa na
waraka wa Elimu Na. 1& 2 wa 2002 urejeshwe na uimarishwe
bila kuchelewa kuasnzia Darasa la kwanza, la pili na la Tatu ambayo
Mwalimu Mkuu siku zote anayo madaraka ya kukalilisha, kama
mwanafunzi hajazijua “K” 3: kusoma, kuandika na kuhesabu.
5.2 Tume ya Mhe. Waziri Mkuu ifanye
kwanza REJEA ya maandiko ya Wizara ya Elimu niliyoyataja akatika 4(a) na
(b) hapo juu yaliyomo maboresho
ya elimu ya 2002-2005
yaliyofanikisha kufaulu vizuri katika Elimu ya Msingi na
Sekondari miaka ya 2004-2007; badala ya
kutumia muda mwingi na fedha n=yingi kugundua upya gurudumu.
5.3 Taasisi ya Elimu
Tanzania ( Tanzania Institute of Education –TIE) iagizwe
na iachiwe kutekeleza wajibu wake wa kisheria chini ya Sheria ya
Elimu ya 1995 wa kuandaa na kuboresha mitala.
5.4 Wanasiasa tuache kuamua
bila kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri w kitaaluma kuhusu Elimu ya
Taifa letu.
Kutokana na uamuzi mbaya na
kuchelewa kuchukua hatua ya marekebisho kila inapobidi; Elimu yetu
imerudi ilikokuwa kabla ya mwaka 2000. Rika zima la kielimu
limepotea!!!sasa tunavuna kilichopandwa vibaya. Kwa hiyo TUJISAHIHISHE kwa
kuacha kuingilia na kuamua bila kuzingatia utafiti na ushauri fwa
kitaaluma ili tusije kuumbuliwa tena na matokeo mabaya kama
hayo ya kidato cha Nne ya mwaka 2012. Aidha inafaa matokeo ya
mitihani yawe yanatangazwa kwa uwazi hata kama ni mabaya kwa
sababu, narudia “ anayeficha maradhi kifo
kitamuumbua”
Wasalamu
Joseph J Mungai MB mstf
MDAU WA ELIMU
No comments:
Post a Comment