masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, February 24, 2013

Watu wawili wanusurika kifo katika ajali




WATU wawili wamenusurika kifo alfajiri ya kuamkia jana baada ya magari yao kupata ajali katika maeneo ya CCDB ya zamani katika Manispaa ya Iringa.

Ajali hiyo imehusiha magari mawaili yenye namba za usajili T 319 AFL aina ya Raver 4 na T 510 AYU Cresta ambapo chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni Raver 4 iliyokuwa katika mwendo kasi ilihama njia na kuruka katika ukingo wa barabara kisha kupanda kwenye gari lililokuwa likipita upande wa pili.

Akielezea tukio hilo dereva wa Cresta Cervin Kaduma alisema wakati akitokea Kihesa kwenda mjini alikubwa na dhahama hiyo baada ya kuvamiwa na gari hilo lililomfuata upande wake.

Alisema magari yote hayakuwa na abiria japo kuwa dereva wa Raver 4 akishikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.



No comments:

Post a Comment