masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, February 5, 2013

Tuwafikie Tanzania kujenga maktaba vijijini


KUTOKANA na kushuka kwa elimu vijiji, asasi siyo ya kiserikali ya Tuwafikie Tanzania imebuni mbinu ya kukabiliana na tatizo hilo ili kukuza kiwango cha elimu vijijini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa asasi hiyo Bovan Mwakiambiki alisema wanatarajia kujenga makta vijijini zitakazosaidia wanafunzi na watu mbalimbali kujisomea kwa muda wote watakaoamua kusoma kitabu chochote.

Mwakiambiki alisema asasi yake ilifikia uamuzi huo kutokana na kuwa kwa kiwango kikubwa watu wa vijijini kieleimu wamesahaulika na kusababisha kuwa nyumba tofauti na maeneo mengine.

Alisema mpango huo unaanza kutekelezwa katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kwa kujenga maktaba katika kijiji cha Lugako Kata ya Ilole Tarafa ya Mazombe ambapo tayari taratibu za ujenzi zinaanza kwa kuwa wamekwisha kupata eneo.

“Tunaanza na madarasa mawili ambayo kila darasa litabeba watu 50 ikiwa ni mwanzo tu wa utekelezaji lakini katika ujenzi huo tunashirkiana na kampuni ya ujenzi ya Costan (Costan Company Limited) iliyopo jijini Dar es Salaam.

Alisema wamechagua kijiji hicho kujenga maktaba hiyo kwa kuwa asasi bado ni changa kiasi cha kutoanza vijiji vya ndani zaidi ili kurahisisha utendaji na utekelezaji uimarishaji hadi pale itakapokuwa imekomaa kuingia ndani zaidi.

“Katika utafiti tulioufanya tumeona Iringa ina muamko wa elimu zaidi kuliko sehemu zingine ndiyo maana tunaanza kujenga maktaba hiyo kwenye Mkoa huu ili Mikoa mingine ijifunze kupitia Iringa baada ya maktaba kuanza kutumika” alisema.

Alisema hiyo ni moja ya uhamasishaji wa elimu kwa watu mbalimbali pamoja na wadau mbalimbali ili waweze kutoa michango yao katika kuinua kiwango cha elimu nchini.

“Maktaba tunayojenga Iringa ni ya kwanza katika utekelezaji wetu wa uhamasishaji nchini na baada ya kukamilika kwake itafuatiwa na ile tutakayojenga Ileje mkoani Mbeya. Leongo letu ni kukamilisha nchi nzima” alisema.

Asasi ya Tuwafikie Tanzanzania yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam intarajia kutumia jumla ya shilingi 23,288,000/= milioni katika ujenzi wa maktaba hiyo huku bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania wakiahidi kuchangia viatabu vya ziada.

No comments:

Post a Comment