MTU aliyepotea katika kijiji cha
Madege kata ya Idete Wilaya ya Kilolo kwa imani zinazosadikika kuwa ni za
kishirikina amepatikana katika mazingira ya kutatanisha akiwa na hali mbaya.
Kutokana na tukio hilo, mtu mmoja
anayejulikana kwa jina la Limitel Mbombwe amekamatwa na wanachi akituhumiwa kwa
kuhusina na kupotea kwa mtu huyo.
Akizungumza katika mkutano wa
dharula katika kijiji hicho, Mwenyekiti wa kijiji hicho Philimino Msuva alisema
Amuru Kiwone mkazi wa kijiji hicho aliripotiwa kupotea katika mazingira ya
kutatanisha Februari 3 Mwaka huu akiwa nyumbani kwake jambo lililosababisha
kuitisha msako wa kila mahali.
Alisema wakati wanakijiji
wakiendelea na msako, zilianza fununu za mpotevu kuonekana katika nyumba ya
Mzee Mbombwe ambaye ni jirani yake hali iliyowafanya wananchi kutoa msimamo
kuwa siku inayofuata wataanza kuingia nyumba hadi nyumba kumtafuta mtu huyo.
Kufika Februari 6 Mwaka huu,
mpotevu alikutwa asubuhi akiwa hajiwezi huku aliwa hana nguo nje kidogo na
yumba ya mtuhumiwa wa tukio hilo
bila kuongea chochote ndipo alipochukuliwa na kupelekwa katika huduma za afya
na kutoa taarifa kwa wananchi kuwa zoezi la utafutaji lisimame kutokana na
kupatikana kwa aliyekuwa akitafutwa.
Akizungumzia juu ya upatikanaji
wake kaka yake Amuru (aliyepote) Osward Kiwone alisema anapoamka asubuhi
kuangalia upande wa juu jirani na mtuhumiwa alimuona mdogo wake akiwa amelala
huku akiwa mtupu.
Wakati wa mkutano huo ambao watu
walifurika kusikiliza namna ilivyotokea, mke wa mtuhumiwa Bi Lena Kihongosi
alithibitisha kuonekana kwa kiwone aliyekuwa akitafutwa katika sehemu anayoishi
mumewe.
“Naomba ulinzi kwenu watu wote
mliofika hapa kwa ajili ya tukio hili. Mwenzenu mumewangu sikai naye nyumba
moja japo kuwa kuna nyumba mbili sehemu moja. Amejitenga nami lakini wakati
watu wakiwa wameacha shughuli zao kwa ajili ya kumtafuta jirani yangu, wajukuu
wangu walikuja walikia kutoka sehemu ambayo mume angu anaishi. Nilipowauliza
wanalilia nini, waliniambia kuwa wamemuona mtu tunayemtafuta na walipotaka
kumuuliza babu yao
akawapiga kuwa wasimwambie mtu yeyote” alisema.
Wakati hayo yakizungumzwa binti
yake aliyejitambulisha kwa jina la Sikunena Mbombwe alithibitisha tukio hilo kuwa ni la kweli
kutokana na vitendo anavyotendewa na baba yake huku watoto wake wakiwa
mashahidi.
“Hilo suala ni la kweli. Watoto wangu wawili
waliniambia kuwa wamemuona anakoishi Baba yangu. Lakini kutokana na vitendo
anavyotendewa mama yangu na ninavyotendewa mimi na Baba huyu vinadhihirisha
wazi kuwa ni vya kishirikina. Huu mzee wetu amekuwa kama
simba kwani mara kadhaa akitutendea kitu kibaya anatutishia kuwa tutakufa.
Siwezi kusema yote kwa sababu hapa kuna watoto na watu wazima pia ila ukweli
ndio huo” alisema.
Katika hali ya kushangaza, mtoto
wa miaka minne ambaye ni mjukuu wa mzee huyo Wini Kisumbi bila kuogopa watu
alieleza kuwa alimuona mtu aliyepotea nyumbani kwa babu yake akiota mto.
“Nilimuona Amuru kwa babu anaota
moto wakati watu wakiwa wanamtafuta. Nilipomuuliza babu kuwa mbona nimesikia
kuwa wale watu pale ng’ambo wanamtafuta huyu babu akanipiga akasema tusimuite
Amuru ila tumuite “Mang’inya”. Nilikuwa na mwenzangu akasema tunakenda
kumwambia mama halafu akatupiga kuwa tusiseme. Ila ni kweli alikuwa mwenyewe
tunamfahamu vizuri kwa sababu ni jirani yetu” alisema mtoto huyo.
Alipopewa nafasi ya kujitetea Mbombwe
alishindwa kukataa na kutiwa hatiani jambo lililowafanya wananchi kumkamata
mbele ya uangalizi wa serikali na kufikishwa maktika ofisi ya kata hiyo kwa
mahojiano zaidi.
Naye mwenyekiti wa kijiji hicho
Philimino Msuva akiongea katika mkutano huo alisema matukio kama
hayo hayana budi kukomeshwa kwa sababu yanarudisha maendelea ya watu nyuma.
Tukio la kupotea kwa mtu katika
kijiji hicho si la kwanza kwani aliwahi kupotea mwanafunzi wa shule ya msingi
na mifupa pamoja na fuvu lake
kupatikana katika shamba
la miwa la mtu mmoja wa kijiji hicho.

No comments:
Post a Comment