masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, February 14, 2013

MBUNGE ATOA MSAADA SHULE YA CHEKECHEA

Mwalimu Eva Mtete akipeana mkonona mbunge Chiku Abwao baada ya kusoma taarifa fupi ya shule

Mbunge Abwao akikabidhi fedha za shilingi 100,000/= kuisaidia shule

Mbunge Abwao katikati katika picha ya pamoj na kamati ya shula


MBUNGE wa viti maalum Chiku Abwao (CHADEMA) ametoa msaada wa shilingi laki moja (100,000/=), viti 6 na meza 2 katika chule ya Chekechea ya Mtaa wa Barabara ya Dodoma TRM (DO/R/TRM) iliyopo katika Manispaa ya Iringa ili kuiwezesha kupiga hatua mbele kutokana na changamoto inayokabiliwa nazo.

Abwao alito msaada huo jana katika kikao cha Kamati ya shule kilichofanyika shuleni hapo baada ya kumuomba katika kikao hicho.

Akikabidhi msaada huo Abwao alisema wazazi na walezi wasikwepe majukumu ya kulea familia zao na kuwajibika kwa kila kitu hususani katika masuala ya elimu ili kuwasaidia watoto kupata elimu itakayowakomboa maishani mwao.

“Nimeziona changamoto zinazoikabili shule hii hasa katika uendeshaji kuwa mgumu. Changamoto hizi zitakwisha endapo wazazi na walezi hawatakwepa majukumu yao” alisema Abwao.

Alisema kuna masuala ambao yanapaswa kusimamiwa na serikali moja kwa moja lakini mengine ni jukumu la wazazi na walezi.

Alisema kutokana na uendeshwaji wa shule kuwa mgumu, kuna haja ya wazazi kuongeza kiwango cha michango angalau kufikia shilingi 5,000/= hasa katika masuala ya malipo ili mwalimu anayefundisha aweze kupata chochote kwa ajili ya kununulia sabuni.

Awali akisoma taarifa fupi ya shule hiyo, mwalimu wa shule hiyo Eva Mtete aliseuma shule inakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo za uchakavu wa jingo ambalo ni la muda mrefu, upungufu wa madawati pamoja na wazazi au walezi kuchelewesha wazazi kituoni.

Hata hivyo alisema ulipaji wa karo bado ni mgumu kutokana na wazazi na walezi kudai kuwa hawana uwezo jambo linalokwamisha maendeleo ya shule hiyo ambapo karo inayolipwa kawa sasa ni shilingi 3,000/= kwa mwezi kwa kila motto.

Katika muhula wa kwanza kwa mwaka huu, shule hiyo imesajili watoto 41 ambapo waliorudia ni 19 huku wapya wakiwa ni 22 pungufu ya watoto wa mwaka jana ambao walikuwa jumla yao 53.

No comments:

Post a Comment