masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, February 14, 2013

Mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi avurumusha matusi mahakamani


KWA mara nyingine mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten Daud Mwangosi amefikishwa leo mahakamani akiwa amejifunika kichwa hadi miguuni.

Pasificus Cleophace Simon mtuhumiwa wa mauaji hayo mwenye namba G 2573 amefikishwa mahakamani katika gari la mahabusu (karandinga) kama watuhumiwa wengine tofauti na siku za mwanzo alipokuwa akifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari.

Mwendesha mashtaka wa serikali Adolf Maganda aliambia mahakama jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa Consolata Peter Singano kuwa upelelezi haujakamilika na hivyo kurudishwa rumande hati 28 Februari Mwaka huu.

Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani hapo kwa gari namba DFP 2175 pick up akiwa katika ulinzi mkali huku waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika kupigwa jambo lililoamsha hisia tofauti miongoni mwa wananchi wengi mkoani hapa.

Katika hali isiyo ya kawaida, mtuhumiwa huyo mwenye namba G 2573 akiwa mahakamani hapo amevurumusha matusi ya nguoni kwa waandishi wa habari kuwataka wasimpige picha huku akijidai kuwa muda si mrefu ataachiwa na kupambana na waandishi mitaani.

Pasificus akiwa na jazba alisikika akisema “mtapiga picha sana mtakavyo lakini hamjui kama kesho tu nitatoka halafu tupambane mitaani huko. Nawaona sana mnaonipiga picha tutakuja kukutana tu” alisema
mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo kuzuiwa kupiga picha kwa waandishi kunaendelea kwa baadhi ya askari kwa kile walichokuwa wakitumia amri kwaandishi kutokusimama katika maeneo ya mahakama wakieleza kuwa sehemu hizo hazitakiwi kusimama jambo alililowafanya waendesha mashtaka kuwakemea askari hao kuwa wapo kinyume na taratibu za mahakama.

Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka jana katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

No comments:

Post a Comment