| Kibaso Msimbiti mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Lyasa anayewatafuta ndugu zake ili afahamiane naye. |
Kibaso Msimbiti mwanafunzi wa
shule ya sekondari ya Lyasa iliyopo Kata ya Ifunda Wilaya Iringa hajawahi
kumuona baba yake mzazi wala ndugu zake wa upande wa baba yake tangu kuzaliwa
kwake kutokana na kufiwa na Mama yake mzazi akiwa bado mdogo.
Akiongea na gazeti hili shuleni
hapo, Msimbiti ambaye kwa kabila ni Mkurya alisema anamtafuta baba yake mzazi
ambaye hata hivyo jina lake
halifahamu .
Alisema kuwa amelazimika kuongea
na gazeti hili ili kwa ndugu yeyote atakayekuwa anamfahamu aweze kumtafuta ili
wafahamiane hata yule atakayekuwa anamfahamu baba yake mzazi aweze kumsaidia
ili kujua alipo.
“Kwa tetesi ninazozipata kutoka
kwa ndugu wa marehemu mama nimeambiwa kuwa baba yangu ni fundi magari
(mechanic) ambaye ni mwenyeji wa kijiji cha Komge – Musoma” alisema Msimbiti.
Amemtaja marehemu mama yake kuwa
alikuwa anaitwa Pelagia Mhelela ambaye alifariki yeye akiwa bado mdogo.
Hata hivyo amemtaja ndugu wa baba
yake mzazi kwa jina la Mama Jose Msimbiti ambaye ni mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam .
“Baada ya mama yangu kufariki
nilichukuliwa na mapadre wa Kanisa Katoliki hapa Lyasa ambao hadi leo wananilea
na kunisomesha lakini natamani sana
kuwafahamu ndugu zangu kwa upande wa baba kwani hadi leo simfahamu hata mmoja”
alisema.
Msimbiti ambaye kwa sasa ana umri
wa miaka 18 anawaomba wasamaria wema wanaomfahamu baba yake na ndugu zake ili
aweze kuonana naye huku akitoa mawasiliano yake kuwa ni 0766-070925 na namba ya
mlezi wake Padre Richard Chatila 0787-498942
No comments:
Post a Comment