| Mratibu wa Baraza la vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (BAVICHA) Aidan Salehe akiongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa Embalasasa Motel. |
Waziri wa fedha na uchumi William
Mgimwa pamoja na Waziri William Lukuvi wamelalamikiwa kuwatesa wananchi katika
majimbo yao kutokana na utaratibu wao mbovu wa
kuwatelekeza bila kukumbuka kukutana nao ili kusikiliza matatizo yao .
Haya yamezungumzwa leo na Aidan
Salehe mratibu wa baraza la vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA)
alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya mahangaiko ya wananchi wa
majimbo ya Kalenga na Isimani kutokana na upatikanaji wa pembejeo za kilimo.
Salehe amesema mfumo mbovu wa
chama cha mapinduzi (CCM) ndio unaowafanya viongozi hao kuwatelekeza wananchi
wao bila kujali matatizo wanayokumbana nayo.
Samesema kutokana na mfumo huo,
mawakala wa pembejeo ndio wanaoonekana kama
ndio wenye dhamana ya kusambaza pembejeo na kugeuza biashara zao hali
inayowatesa wananchi katika kufanikisha kaulimbiu ya “Kilimo kwanza”.
“Mfumo mbovu wa serikali ya CCM
wa kuwaachia mawakala kusambaza mbolea umeleta matatizo katika Wilaya ya Iringa
(V). Hii inatokana na mawakala kuuza mbolea kwa bei ghali sana
tofauti na utaratibu wa serikali kutoa mbolea ya ruzuku kama kama
wanavyojinadi neon lao “kilimo kwanza” amesema Salehe.
Kutokana na lawama za mratibu
huyo, imebainika kuwa pembejeo hizo katika Wilaya hiyo mbolea ya DAP inauzwa
shilingi 80,000, Minjingu shilingi 40,000, Urea 70,000 na Mbegu kilo 10 inauzwa
shilinigi 45,000 na kutofautiana na bei za mjini ambapo DAP inauzwa shilingi
75,000, Minjingu 20,000, Urea 65,000 na Mbegu kilo 10 ni shilingi 40,000.
Salehe amesema CCM wanakiuka
ilani yao ya
uchaguzi ya mwaka 2010, ibara ya 31 kifungu kidogo a, b, c, na d.
Katika ilani hiyo inaeleza kuwa
CCM wataanzisha Benki ya kilimo ili kutoa mikopo kwa wakulima kukipatia kilimo
fedha za kutosha kwa kuhakikisha kwamba bajeti ya serikali haiwi kuzuizi cha
maendeleo ya kilimo nchini pamoja kuongeza upatikananji na utumiaji wa pembejeo
za kilimo hususani mbolea, mbegu na miche bora na kuweka mfumo utakaohakikisha
upatikanaji wa pembejeo hizo kwa wakulima.
Salehe amesema wasimamizi wa ilani
hiyo katika majimbo ya Kalenga na Isimani, wameshindwa kusimamia kilimo na
badala yake wamegeuka kuwa mateso na mzigo kwa wananchi waliowachagua.
“Kutokana na wabunge hawa
kushindwa kusimamia ilani ya uchaguzi, Katiba ya nchi, Katiba yao
ya CCM ambayo wanatakiwa wasimamie na kwa kuwa wakulima ndio wahanga kwani
waliwachagua kupitia ilani yao ”
amesema
Hata hivyo amesema mapendekezo ya
BAVICHA wanataka serikali iwatangazie wananchi kuvunja kaulimbiu ya kilimo
kwanza kwa kuwa haina tija kwa wakulima.
“Tunapendekeza kuwa, serikali
iwatangazie wananchi kuvunja kwa kauli mbiu ya “kilimo kwanza” kwani haina
msaada kwa wananchi wakulima walio wengi vijijini, wananchi wawatathimini
wabunge wao na kuitathmini ilani ya CCM na wajiridhishe kuwa walidanganywa ili
ifikapo kipindi cha uchaguzi wasiwapigie kura kuanzia uchaguzi wa serikali za
mitaa na uchaguzi mkuu pamoja na maofisa kilimo wa Mkoa, wilaya pamoja na
mabwana shamba wote wawajibishwe kwa kushindwa kuchukua hatua za kurahisisha
upatkanaji wa pembejeo kwa wakati” amesema.
Amesema hakuna haja ya CCM
kujinasibu kuwa inatekeleza kilimo kwanza wakati wakulima wanakosa pembejeo.
Aidha amemkumbusha Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kuhakikisha anatekeleza kwa
vitendo utoto wake wa mkulima kwa
vitendo badala ya kuzungumza kwa maneno.
“Bavicha tunamtaka Waziri Mkuu
Mizengo Pinda kutekeleza kwa vitendo kifungu cha 52 cha Katiba ya nchi yetu juu
ya utekelezaji wa shughuli zake za kila siku kwani ameshindwa kusimamia kilimo
nchini mwetu ambacho kimegeuka mradi wa wachache” amesema
Hata hivyo ameitaka serikali
kupeleka chakula mara moja katika vijiji vya Kipera, Kiwele, Mgera katika jimbo la Kalenga pamoja na vijiji vya
jimbo la Isimani karibu vyote pamoja na kuitaka CCM kuiga ilani ya CHADEMA ya
2010 – 2015 katika kifungu 4.1.1 ambayo inasema “CHADEMA inaamini katika kilimo
bora cha kisasa, na kuwa kilimo kwa sasa na muda mrefu ujao ndio nguzo kuu ya
uchumi kwa Tanzania. CHADEMA inaamini pia kwamba ili kilimo kiweze kukua
kinavyostahili na
Serikali ya CHADEMA itaangalia
uwezekano wa kuanzisha kilimo cha mijini (urban farming) hasa katika mawazo ya
bustani za mboga na matunda”.
No comments:
Post a Comment