MWANDISHI wa habari wa
gazeti la Mtanzania Oliva Motto amenusurika kupigwa mahakamani na katibu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi Jacob Nkomola
aliyefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili.
Tukio hilo
limetokea leo katika Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa,
kwa kumvamia Mwandishi wa habari kwa kile alichokiita ni hasira ya kesi yake.
Kizaa zaa hicho
kiliianza mara mwandishi huyo alipokuwa akipiga picha mahakamani hapo ikiwa ni
sehemu yake ya uwajibikaji katika kazi yake.
Nkomola alifikishwa mahakamani
hapo kujibu shtaka linalomkabili la kutishia kuua kwa maneno, kinyume na sheria
kifungu namba 89 kifungu kidogo “A”.
Akimsomea shitaka mahakamani hapo Hakimu Zakaria
Mushi alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo
Oktoba 3 mwaka jana (2012) katika eneo la Mkombwe, ambapo alimtishia Alexandel
Tweve mkazi wa Mafinga.
Mtuhumiwa alikana shtaka hilo kisha hakimu akutoa masharti ya dhamana
ya ahadi ambayo inathamani ya shilingi laki mbili (200,000/=), na adhaminiwe na
mtu mmoja atakayetambulishwa kwa barua kutoka katika ofisi ya serikali ya
kijiji au Kata.
Kupitia masharti hayo mshatakiwa alikuwa na
mdhamini ambaye hakukidhi vigezo vya kuwa na barua ya uthibitisho kutoka katika
ofisi za serikali ya kijiji na hivyo kuzuiliwa kwa muda wa saa moja akiwa chini
ya ulinzi.
Kesi imeahirishwa hadi 30
Januari mwaka huu itakapotajwa tena na hakimu alimtaka mstaki wa kesi
hiyo kufika na mashahidi wake aliowaorodhesha
Katika hatua nyingine
mara baada ya kesi kuahirishwa na baada
ya mwandishi wa gazeti hilo
kutoka nje kwa ajili ya kupiga picha, mtuhumiwa alimfuata mwandishi na kumkuda
akihoji ridhaa ya mwandishi huyo kupiga picha.
“Kwa nini unanipiga picha? Nani amekuruhusu unipige
picha, kwanza wewe ni nani? Umepokea rushwa huko uje uniandike mimi, na nitaona
kama habari hiyo itatoka,” Alihoji Katibu huyo.
Akijibu maswali ya mtuhumiwa huyo mwandishi
alisema “Mimi ni mwandishi wa habari, ninafanya kazi kwa maadili, sijakurupuka
ndiyo maana nawajibika. Hii ni kazi yangu huwezi kunifundisha wewe leo hapa
mahakamani” alisema mwandishi huyo
Hatua hiyo iliwashangaza watu waliohudhuria kesi
hiyo katika viunga vya mahakama wakihoji mamlaka ya mtuhumiwa kumfuata umbali
wa hatua zaidi ya saba mwandishi, huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi kwa kuwa
bado alikuwa anashikiriwa kutokana tuhuma pamoja na kutokidhi vigezo vya
dhamana yake.
Mwandishi huyo alikimbilia kwa hakimu wa
mahakama hiyo akitaka msaada juu ya tujkio hilo,
na ndipo hakimu Mushi alimtaka mwandishi huyo kufika kituo cha polisi kutoa
taarifa ya tukio hilo.
Akiwa njiani Mwandishi alimpigia simu Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Mufindi Cosmas Kaguo ambaye alimuomba mwandishi kuonana naye
kabla ya kufika katika kituo cha Polisi cha Mafinga.
Hatua ya mwenyekiti wa CCM Kaguo kukutana na
mwandishi huyo kabla ililenga kufanya kikao cha dharura jamba ambalo
alifanikiwa kuitisha kikao hicho na kamati ya siasa na kuomba radhi juu ya
tukio lililotokea, na baada ya muda wa dakika 20 Katibu wa CCM (Mtuhumiwa)
aliingia katika moja ya ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, iliyopo
katika ukumbi wa mikutano na kuomba radhi juu ya kile alichokifanya katika
viunga vya mahakama.
Ombi la mwenyekiti wa CCM Wilaya, lilikubaliwa
na mwandishi huyo kwa kusitisha hatua yake ya kufungua kesi katika kituo cha
polisi Mafinga.
Akitoa utetezi wake, mtuhuimiwa huyo alisema
“Ninaomba unisamehe sana
Oliver, unajua kesi yangu hii niya kisiasa, na kukufanyia hivyo ni hasira baada
ya mtu anayenituhumu kutumia njia mbalimbali za kuniangamiza, ninajua
nimekukwaza wewe, lakini pia nimeidhalilisha taaluma yako, ninakuomba
unisamehe,” Alisema Nkomola.
Hata hivyo baadhi ya wanasiasa Wilayani humo
walisema katibu huyo amekuwa akitumia vibaya wadhfa alionao, na kujisahau kama
kuna mikono ya sheria, na kuwa nguvu ya kufanya vurugu katika chombo hicho cha
mahakama ambacho ni muhimili mkuu wa serikali, ni kutokana na jingo la Mahakama
hiyo kuwa ni mali ya chama cha mapinduzi.
“Angekuwa mtu mwingine aliyefanya vurugu
Mahakamani angechukuliwa hatua pale pale, kufanya fujo mbele ya mahakama, tena
mahakimu wanaona, si jambo la mdhaha, ni kuidharau Mahakama, laki amefanya vile
kwanza akijua yeye ni kiongozi mkubwa wa chama Wilayani humo, lakini pili, ni
juu ya jingo lao, anaona kama anayo haki ya kufanya chochote yeye kama baba
mwenye nyumba wa Mahakama hiyo, lakini si sifa ya kiongozi bora hata kidogo, na
kusema nitaona kama habari hiyo itatoka inamaa yeye ndiyo anayezuia na kuruhusu
habari?, anataka kutwambia yeye ndiyo mratibu au mhariri wa vyombo vyote vya
habari!” Walihoji.
Kikao cha usuruhishi dhidi ya tukio hilo, kilichukua zaidia
ya saa nzima hadi kumalizika kwake, mwandishi huyo yupo wilayani humo kwa siku
ya tatu sasa, akifuatilia masuala ya elimu kwa wanafunzi wanaoanza elimu ya
kidato cha kwanza, pamoja na changamoto zinazoikabiri sekta ya elimu na Kilimo
Wilayani humo.

No comments:
Post a Comment