masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, January 15, 2013

Leonard arithi mikoba ya Mwangosi

Frank Leonard akiwashukuru wanachama wa IPC kwa kumchagua kurihti nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti Daudi Mwangosi.

Frank Leonard mwenyekiti wa IPC aliyekaa kushoto na Francis Godwin katibu mtendaji aliyekaa kulia wakiwa kwenye viti vyao mara baada ya kuchaguliwa katika nafasi hizo.

Happiness Matanji mara baada ya kuchaguliwa katika nafasi ya kamati tendaji akiwaeleza wanachama wa IPC namna atakavyowajibika katika nafasi yake.

FRANK Leonard amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), akirithi nafasi ya marehemu Daudi Mwangosi.

Marehemu Mwangosi aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten, aliuawa kwa bomu wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa Septemba 2 mwaka jana.

Leonard alichaguliwa kurithi nafasi hiyo juzi katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya M.R mjini hapa.

Wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Jackson Manga (Mwenyekiti Msaidizi), Francis Godwin (Katibu Mtendaji), Janeth Matondo (Mweka Hazina) na Selemani Boki (Mweka Hazina Msaidizi).

Waliochaguliwa kuingia katika Kamati Tendaji ni Happiness Matanji, Selina Ilunga na Tukuswiga Mwaisambe.

Matondo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mweka Hazina, Vick Macha, aliyefariki dunia Oktoba 14, mwaka jana.

Akitoa shukrani kwa wajumbe waliomchagua, Leonard alisema viatu vya Mwangosi vinamtosha, hivyo ataendelea kuvivaa.

“Nashukuru kwa kunipa hii nafasi. Naahidi kuendeleza pale alipofikia Mwangosi na kuendelea kuvaa viatu vyake. Haki ni haki, ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Hayo nitayazingatia katika kazi. Pia kwa kuwa tayari nina uzoefu wa kazi katika chama chetu, nitajitahidi kuwajibika, ili tuweze kusonga mbele kimaendeleo.

“Mtakumbuka baada ya kifo cha Mwangosi tumeyumba kidogo, kwa sababu hilo ni pigo, lakini sasa tukiendelea kufuta machozi tutaendeleza chama chetu,” alisema.

No comments:

Post a Comment