masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, January 15, 2013

Mtwara wana haki ya kuandamana’





JUMUIYA ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Mkoa wa Iringa, wafanyabiashara na wadau wengine wanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara, wameunga mkono maandamano ya wakazi wa mikoa hiyo kupinga usafirishaji wa gesi asilia kutoka Mnazi Bay, Mtwara, kwenda Dar es Salaam.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya bustani ya manispaa jana walisema wamefikia hatua hiyo kutokana na serikali kupuuzia na kuwatukana wananchi wa mikoa hiyo kuwa ni wapuuzi.

Akisoma tamko hilo, mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Mukhaji Namangaya, alisema kisheria na katika hali ya kawaida rasilimali yoyote ile inayopatikana eneo fulani ni lazima iwanufaishe wananchi wanaoishi katika maeneo husika, lakini mtazamo uliopo unalenga kuwadhulumu wazawa.

Alisema kumekuwa na dhuluma nyingi za rasilimali na kuorodhesha miradi mbalimbali ya maendeleo, hivyo ni wakati wa kuhakikisha uzorotaji wa maendeleo haujitokezi tena.

Akitaja baadhi ya miradi iliyosimama kwa kukwamishwa na serikali kuwa ni kuondolewa kwa mashine ya kuvuta maji katika vijiji vya Mitema na Chihanga wilayani Newala kwa madai kuwa ni mbovu hatimaye kupelekwa kutumika mkoa wa Dodoma.

Miradi mingine alisema kuondolewa kwa taa zenye mwanga mkali katika uwanja wa ndege wa Mtwara na kupelekwa katika viwanja vingine katika mkoa wa Arusha, ubabaishaji uliofanywa na serikali juu ya ahadi ya kukarabati Bandari ya Mtwara, kuahirisha ujenzi wa kiwanda cha samaki mkoani Mtwara na hatimaye kwenda kujengwa jijini Dar es Salaam na ubabaishaji wa bei za korosho kupitia utaratibu mbovu wa stakabadhi ghalani bila kuwashirikisha wakulima.

Alisema kusafirisha gesi kupeleka Dar es Salaam ni kuendeleza tatizo la ongezeko la idadi ya watu jijini Dar es Salaam kama vile Wamachinga ambao asilimia kubwa wanatoka mikoa ya kusini.

Naye Rais wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO), William Rufil, alitaka kilio cha watu wa kusini kisipuuzwe kwa kuwa wako sahihi kudai mali yao kulingana na taratibu.

No comments:

Post a Comment