masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, January 7, 2013

Wanawake walilia vitambulisho vya kupigia kura Iringa




Serikali imeombwa kuweka zoezi la kila mwaka la uandikishaji wa vitambulisho vya wapiga kura, kufuatia idadi kubwa ya watu Nchini hususani vijana kushindwa kujitokeza katika zoezi la upigaji kura pindi linapotokea.

Haya yalijitokeza jana wakati Mbunge viti maalum Chiku Abwao (CHADEMA), wakati wa zoezi la kuunda kikundi cha TUJIJENGE cha wanawake wajasiliamali katika kata ya Mwangata Mkoani Iringa, ambapo baadhi ya wanawake hao walidai kuwa, watanzania wengi hawana vitambulisho vya kupigia kura kutokana na baadhi yao kupoteza na wengine kufikisha umri wa miaka 18 hivyo kuwa na haki ya kumiliki kitambulisho hicho kwaajili ya kumchagua kiongozi wanayemuhitaji.

Mmoja wa wanawake hao katika kikundi hicho Rehema Mbetwa, alimuomba Mh. Chiku kulifanyia kazi suala la vitambulisho, ili kuifanya Nchi ya Tanzania kuwa na Demokrasia ya kweli kwa kumfanya kila mwananchi mwenye sifa ya kumiliki kitambulisho hicho kukipata na kuwa na haki ya kumchagua kiaongozi anayemfaa.

“Hata kama viongozi wetu watakuwa wanapiga kelele watu wajitokeze kupiga kura, endapo watu watakuwa hawa vitambulisho vya kupigia kura haitasaidia kitu chochote”, alisema Mbetwa.

Hata hivyo Mbunge huyo alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kudai kuwa endapo Serikali ingekuwa inajali demokrasia, suala la upatikanaji wa vitambulisho lingekuwa ni la kila mwaka, ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki ya kuchagua ama kuchaguliwa.

Mbunge huyo alidai kuwa Suala la upatikanaji wa vitambulisho vya kupigia kura halijafanywa kuwa la kila mwaka kwa maslahi ya kisiasa.

“Kwasababu kunawakati vijana wengi walikuwa hawajali sana masuala ya kupiga kura, wakapoteza vitambulisho vyao huku wengine walirubuniwa na baadhi ya viongozi mbalimbali wakauza vitambulisho vyao, ndo maana sasahivi chaguzi nyingi za marudio unakuta CCM walishinda kwa kishindo kikubwa kutokana na wenye vitambulisho vya kupigia kura sasa hivi ni wazee ambao wapo CCM, huku vijana wengi ambao ni wapinzani hawana vitambulisho.

Aliahidi kulifuatilia suala hilo la vitambulisho ili liwe endelevu kwa kila mwaka, na kudai kuwa endapo hawatalipitisha suala hilo CHADEMA itatumia nguvu ya umma kudai haki hiyo.

Licha ya changamoto ya vitambulisho ,Mh. Abwao aliongeza kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya kisiasa kuwabeba wapiga kura wakati wa kampeni za uchaguzi na kuwapatia vitenge na kofia na kasha kupotea, badala ya kubuni mbinu endelevu za kubadilisha maisha ya mtanzania.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanawake hao walidai kuwa, mkoani Iringa wamesema wengi wao wamekata tamaa kutokana na wanasiasa wengi kuwa waongo na kuwatumia vibaya wakati wa kamapeni na baada ya hapo wanapotea moja kwa moja.

“Kumekuwa na tabia ya wanasiasa kuwabeba wapiga kura na kugawa kanga, kofia na kutoa pesa bila kuwawezesha ili muweze kujitegemea lakini mimi natekeleza ilani ya Chama cha Demokrasia ya Maendeleo kuwawezesha wanawake wenzangu ili muweze kuboresha maisha yenu kuacha tabia ya utegemezi” alisema Abwao.

Alisema matatizo mengi yanapojitokeza wanaopata taabu ni wanawakejambo ambalo limekuwa mzigo mzito kwa sababu ya umaskini.

“Matatizo mengi ya umasikini yanatukumba sisi wanawake, umaskini
unatufanya tuwe watumwa na wanyonge kwa kuwa tunakuwa hatuna kitukinachoweza kutusaidia kutatua matatizo yanayotupata lakini tukiwatunajiweza kiuchumi, tunakuwa tayari kuyatatua matatizo hayo” alisema Abwao.

Alisema adui mkubwa wa wanawake ni umaskini na unyonge ambao unamfanya mtu kufa upesi kwa sababu ya kufikiri bila kupata ufumbuzi.

“Unyonge unatufanya kufa upesi kwa sababu ya mawazo. Adui yetu mkubwa wa wanawake ni umasikini. Tusikubali umasikini hata kidogo” alisema.


No comments:

Post a Comment