masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, January 5, 2013

Mvua yaleta maafa Iringa



MVUA kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana mkoani Iringa, imesababisha zaidi ya watu 20 kukosa chakula na kuharibiwa mali zao majumbani na kwenye maeneo ya biashara katika mtaa wa FFU Kihesa.

Uharibifu huo umetokana na maji kufurika katika nyumba hizo na maduka na hivyo kusababisha hasara kubwa.

 Kwa niaba ya wenzake, mmoja wa waathirika wa mafuriko hayo, Teresia Mwalongo, aliliambia gazeti hili kuwa, katika nyumba yao wamekosa chakula kutokana na maji kujaa ndani, huku baadhi ya mali zao zikipotea kwa kusombwa na maji hayo.

Alisema kuwa ilipofika majira ya saa 11 alfajili, maji yalijaa kwa kasi katika nyumba yao na kuingia kwenye vyumba wanavyoishi hali iliyosababisha uharibifu huo.

“Ilikuwa kama saa 11 hivi, kunapokucha ndipo tulipoona maji yanaingia kwenye vyumba, tukaamuka kuangalia kilichotokea ni nini na baada ya kufungua milango tukaona uwanjani maji yamejaa, ambayo yalisomba baadhi ya vyombo pamoja na vyakula vyetu,” alisema.

Aliongeza kuwa jitihada za kuyatoa maji katika vyumba hivyo ili kuokoa mali zilishindikana kwa kuwa tayari yalikuwa hayana njia za kupita kwa vile miundombinu imezidiwa na kuziba.

Hata hivyo, thamani ya mali zilizoharibika haijajulikana kwa kuwa ilikuwa bado mapema mno.

Ofisa Mtendaji wa mtaa huo, Lucas Wikes, alipoulizwa idadi ya wakazi walioathiriwa na mafuriko hayo, alikuwa mkali na kutaka taarifa hizo zitolewe ofisini hatua iliyowashangaza wananchi hao.



No comments:

Post a Comment