masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, January 5, 2013

Viongozi waombwa kutowatenga wanawake

Mbunge wa viti maalum Chiku Abwao (CHADEMA) akiwa katika maongezi na wanawake wa kikundi cha Tupendane mara baada ya kukiunda. Kikundi hicho kipo katika Kata ya Mivinjeni katika Manispaa ya Iringa.
Wanawake wa kikundi cha Tupendane walipokuwa wakimsikiliza Mbunge wa viti maalum Chiku Abwao (CHADEMA) mara baada ya kuundwa, wakisikiliza taratibu za uendeshwaji wa kikindi hicho.


Wanawake Mkoani Iringa wamewataka viongozi wa nafasi mbali mbali Serikalini hususani Rais, wabunge na madiwani kutowasahau pindi wanapopata nafasi ya uongozi, kwasababu wao ndio wapiga kura wakubwa kuliko wanaume.

Wakiongea  kwa nyakati tofauti  wakati  wa uundwaji wa  kikundi cha wanawake wajasiliamalicha TUPENDANE kilichopo katika kata ya Mivinjeni kinachosaidiwa na Mbunge viti maalum  Mkoani Iringa Mh. Chiku Abwao (CHADEMA), walisema kuwa, viongozi wengi wamekuwa wakiwatembelea wakati wa kampeni za uchaguzi huku wakitoa ahadi tele kwa wanawake na kinamama, lakini wakishapata uongozi hutokomea.

Akiunda kikikundi hicho jana Abwao aliwataka wanawake wajitahidi kuwa wabunifu ili waweze kufanya kazi zenye maendeleo kwa ajili ya kujikomboa wenyewe kiuchumi.

“Wanawake mbumbumbu hawawezi kuwa na maendeleo na badala yake atakuwa anatumiwa na wajanja kwa maslahi yao binafsi. Jitahidini kuwa wabunifu ili msitumiwe na watu wasiowatakia maendeleo” alisema Abwao.

Amesema mwanamke anapodumaa kimaendeleo husababisha familia zao kusambaratika hasa watoto kukimbilia kwenye miji mikubwa kutafuta kazi.

“Wasichana wengi wamekuwa wakikimbia kwenda mijini kutafuta kazi na vijana wamekuwa wakitumia madawa ya kulevya na kusababisha matatizo katika familia kwa sababi nyumba hiyo inakuwa haina maendeleo” alisema Abwao.

Alisema umaskini unaokithiri katika jamii ya watanzania unasababishwa na mipango mibovu ya kimaendeleo ambapo watu wachache wanafaidi rasilimali za nchi bila kuwajali wenzao.

“Umaskini wetu unasababishwa na mipango mibovu ya kimaendeleo kwa kuwa watu wachache wanaamua kutumia rasirimali za taifa kwa manufaa yao binafsi bila kuwajali wengine na kusababisha mfumuko wa bei, ukosefu wa vifaa mbalimbali katika sekta ya afya pamoja na mambo mengi kuwa magumu kwa kwa sababu ya kipato duni cha wananchi” alisema.

Aliwataka wanawake hao kushirikisha waume zao katika maendeleo yao ili waweze kuwapa msaada zaidi.

“Shirikisheni waume zenu katika shughuli mnazozifanya ili waweze kuwaunga mkono na kuwapatia msaada wa kusonga mbele” alisema.

Kwa upande wake Katibu wa kikundi hicho Asia Salehe alisema Abwao ni mwanamke na mwanasiasa pekee anayewajali wanawake kwa kuwataka wawe na maendeleo na hivyo kuwataka wanawake wenzake kutomkatisha tamaa.

“Tumempata mwanamke mwenye kututakia mema kimaendeleo ambaye ni wa pekee, mwanasiasa aliye tofauti na wengine kwa kuwa amekuwa mtendaji wa moja kwa moja” alisema Salehe.

Naye mwenyekiti wa kikundi hicho Husna Ngasi alisema hakuna mbunge aliyewahi kuunda vikundi vya wanawake katika kata hiyo licha ya wanawake kuwa na hamu ya kujiunga katika vikundi.

“Kweli tunamshukuru Mbunge Abwao kwa kutukusanya wanawake kwa ajili ya kutuwezesha. Hakuna Mbunge ambaye aliwahi kutuunganisha kama hivi. Tumpe ushirikiano kwakuwa anaonekana kuwa na moyo wa dhati” alisema Ngasi.

Kikundi hicho kina jumla ya wanawake 32 ambapo kinatarajiwa kuzinduliwa Januari 9 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment