| Hili ni moja ya dampo ambalo limetelekezwa na uchafu katika maeneo ya msikitini Kihesa katika Manispaa ya Iringa. |
MBUNGE
wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) anatarajia kuongoza wakazi wa
mji huo katika operesheni ya siku mbili ya usafi katika Manispaa hiyo yenye ikiwa mpango kabambe wa kuuweka mji katika hali ya usafi.
Manispa hiyo kwa sasa inakabiliwa na hali ya uchafu kupindukia
kutokana na kuibuka kwa madampo mengi ya kutupa taka yasiyo rasimi
yanayotokana na uwezo mdogo wa Halmashauri kuwa na mpango wa kuuweka mji safi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Msigwa amesema
ameliona tatizo hilo na tayari imewaomba msaada wadau mbalimbali
waliojitolea magari, fedha na wengine wakidai watajitolea nguvu zao
katika kufanikisha kazi hiyo.
“Manispaa
inagari moja la kusomba takata, gari hilo limeshindwa kusombaa uchafu
kutokana na kiwango kikubwa cha uchafu kinachozalishwa ndani ya Manispaa
hii, hajuna sababu ya kumlaaumu mtu hii ni kazi ya kijamii,ombi langu ni
kwa wananchi wote tujitokeza kwa wingi kesho kushirikiana na vijana
waliokubali kujitolea kusafisha mji wa Iringa” amesema Msigwa.
Amesema
suala la usafi wa mazingira halina uhusiana na chama chochoite cha
siasa kwa kuwa athari zitokanazo na uchafu yakiwamo magonjw aya mulipuko
hayawezi kuchagua watu kutokana na itikadi za vyama vya siasa.
“Uchafua
ni hatari kwa wakazi wa Iringa hususani kipindi hiki cha mvua,kwani ni
chanzo cha magonjwa ya lipuko na kipindupindu, magongwa ambayo yakitokea
hayatachagua mtu kwa msingi wa itikadi ya chama chake cha
siasa, hayawezi kuangakia mimi Chadema na Yule CCM” amesema Msigwa na
kuongeza.
Amesema
katika kufanikisha hilo tayari watu mbalimbali wamejitokeza kwa wingi
baadhi yao wamejitolea gari zao kutumika kusomba takata,wengine wametoa
fedha na baadhi ya vijana wameahidi kujitolea nguvu zao.
“Ombi
langu kwenu ni kwamba ikiwa mtakuta vijana wakifanya kazi ya usafi wa
mazingira kesho msiwapate wasaidieni ili kw apamoja tuwezi
kufanikiw akuweka mji wetu katika hali ya usafi,siku za nyuma Manispaa
ya Iringa ilikuw amiongoni mwa miji iliyoongoza kwa usafi Tanzania
lakini kwa sasa umetupwa mbali nah ii sijui sababu yake ninini”alisema
Msigwa na Kuongeza:
“Na
huu si wakati wa kujadili kutafuta nani kasababisha bali ni wakati wa
kushirikiana kuweka mji katika hali ya usafi na ndipo tuanza kuona
wahusika wanasitahili kufanya nini” amesema.
No comments:
Post a Comment