masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, January 2, 2013

Wanawake wa Mafuruto wanufaika na mkopo



IKIWA ni wiki moja tu kupita baada ya Mbune wa viti maalum Chiku Abwao (CHADEMA) kuzindua kikundi cha wanawake cha Mafuruto, wanawake hao wameanza kunufaika na mkopo kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.

Akitoa mkopo kwa wanawake hao mwanzoni mwa mwaka huu alisema yeye anataka kuwa tofauti na wanasiasa wengine ambao huishia kuahidi na kupotea bila kutekeleza.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwawezesha wanawake waweze kujitegemea na kuachana na tabia ya kusubiri wakati wa kampeni na kupewa vitenge kama kishawishi cha kupiga kura.

“Hii tabia ya kusubiri vitenge kwenye kampeni iishe kwa kusababu mktakuwa mnauwezo wa kujitegemea” alisema.

Abwao alisema kuwahadaa wanawake ni kuyumbisha maendeleo kwa kuwa wanawake wana mchango mkubwa wa kuleta maendeleo kwa taifa.

Hata hivyo alisema nchi inakosa viongozi bora kwa sababu ya watu wenye pesa wanawatumia maskini kuwahonga ili wawachague.

“Tunakosa viongozi bora kwa sababu tunakuwa tegemezi nakutoa mwanya kwa watu wenye fedha kututumia sisi maskini kwa kutuhonga ili tuwachague” alisema Abwao.

Naye katibu mtendaji wa kikundi hicho Yusta Udamwa alisema endapo taifa litatambua mchango wa wanawake, uchumi utasonga mbele.

Aliwataka wanawake wenzake waachane na majina ya akina mama siyawezi kwa kushindwa kusimama kwa miguu yao wenyewe na kusubiri kuhongwa wakati wa kampeni.

“Hatutaki mwanamke anayeitwa mama siyawezi kwa kushindwa kuwa na msimamo na kutegemea hongo wakati wa kampeni. Tumtumie mwanamke mwenzetu ambaye anatujali” alisema Udamwa.

Akitekeleza ilani ya chama chake, Abwao alitoa mkopo wa shilingi 350,000/= ambapo wanakikundi walipendekeza wapewe watu 7 kwa kiwango cha shilingi elfu 50 kila mmoja na kuwataka waliopewa mkopo huo kuwa waaminifu ili wengine waweze kupata fursa ya kunufaika.

No comments:

Post a Comment