masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, January 10, 2013

Viongozi wa CCM wakimbia operesheni ya usafi Iringa

Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akipakia uchafu kwenye gari wakati wa operesheni ya kufanya usafi aliyoiongoza katika Manispaa ya Iringa.

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa waliojitokeza kufanya usafi katika operesheni ya usafi iliyoongozwa na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa wakikusanya uchafu kwa ajili ya kupakia kwenye magari.

Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwa juu ya gari akiweka uchafu vizuri ili wakati wa kusafirisha usianguke njiani. Hili limefanyika leo katika eneo la uchafu uliopo katikakati ya kata ya Kitanzini na kata ya Mshindo jana.

MADIWANI na viongozi wa Mitaa katika Manispaa ya Iringa wamekwepa kushirikiana na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa katika operesheni ya usafi iliyoanza leo ndani ya Manispaa hiyo.

Wakati watu mbalimbali wakijitokeza kushirikiana na Mbunge huyo kufanya usafi katika Kata ya Kitanzini, wakazi wa mitaa hiyo wameshindwa kushirikiana na wenzao kwa kile walichosema viongozi wao wa mitaa waliwakatalia.

Mama mmoja ambaye alikuwa akichambua mboga nje ya nyumba jirani na walipokuwa wakipakia uchafu kwenye gari ambaye hata jina lake hakutaka kulitaja kwa kile alichosema sensa ilishapita alisema anawashangaa watu kujipendekeza katika mitaa yao wakati viongozi wao wa mitaa hawakuwaambia lolote.

“Unaniuliza jina la nini wakati sensa ilishapita na idadi ya watu ilishatangazwa. Viongozi wetu wa wa mitaa walisema tusiende kwa sababu hiyo kazi ya kufanya usafi alitangaza Mbunge ila wakitangaza madiwani wetu tujitokeze kwa wingi” alisema mama huyo.

usafi huo ukiendelea kufanyika madiwani wa Kata za Kitanzini na Mshindo hawakujitokeza licha ya kuwa sehemu hiyo ambayo ilisheheni uchafu wenye uzito wa tani 97 katika mitaa ya Ubena, Madrasat na Mtunduruni mpakani mwa Kata ya Kitanzini na Kata ya Mshindo huku wakionekana madiwani wawili tu wa Kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi na diwani wa viti maalum Suzan Mgonukulima (CHADEMA).

Akizungumza wakati wa kufanya usafi, Diwani wa Kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi (CHADEMA) ameonesha masikitiko yake juu ya madiwani wenzake kutoshiriki zoezi la kuiweka Manispaa katika hali ya usafi.

“Baada ya kufika hapa nimesikitishwa sana kwa kuwa diwani wa kata hii tunayofanya usafi haonekani” amesema Nyalusi.

Amesema kitu cha kushangaza ni pale uchafu unaporundamana katika kata yake na kushindwa kuuchulia hatua mpaka Mbunge kuamua kuingilia kati jambo ambalo ni aibu kwa Taifa.

“Kama yeye ni kiongozi wa eneo husika ameshindwa kuudhiti uchafu huu hadi Mbunge kuingilia kati, hii ni aibu kwa Taifa. Hii inaonesha wazi kuwa viongozi wa CCM uwezo wao ni mdogo. Kwanza wanatumia muda mwingi kujadili mambo ya chama na kushindwa kujadili matatizo ya wananchi wa maeneo yao. Mahindi sasa hivi gunia 1 linauzwa shilingi 105,000/= wao wakiwa katika mijadala ya chama badala ya kujadili hali ngumu ya watanzania. Wanafunzi wa darasa la kwanza wanatakiwa kuchanga shilingi 75,000/= wao wakiwa katika mijadala ya chama na kushindwa kujadili hilo” amesema Nyalusi.

Diwani wa viti maalum Suzan Mgonukulima ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Manispaa amesema, kama nchi hii haitakuwa na ushirikiano kama inavyoonesha kwa madiwani wa Manispaa hiyo watu watakuwa mbumbu kwa kuwa hawatakuwa na viongozi wenye muamko wa maendeleo.

Naye Hezlon Lusapi amesema kutokana na uchafu uliokithiri ndani ya Manispaa unatokana na mikakati mibovu ya Mkurugenzi wa Manispaa.

Kwa upande wake Mbyunge Msigwa alisema cha msingi watu wanatakiwa kuwa marafiki wa usafi na kutosubiri kuambiwa wafanye usafi.

Amesema kutona na taifa kulelewa kwa malipo zaidi, mwitikio wa watu waliofika wanastahili pongezi kwa kuwa waneonesha uzalendo bila kutanguliza malipo.

“Taifa hili limelelewa kwa malipo. Hata ukisema mtu ajitolee kufanya kazi ambayo kwake ina manufaa anataka kulipwa. Hasa hili suala la usafi watu wanataka kulipwa licha ya kuwa wengine wametoka mbali kuja kufanya kazi hapa la wenyeji wa hapa ambao uchafu huu wanautupa wenyewe wanataka kulipwa. Waliofika hapa bila kutaka malipo ndiyo wazalendo wa kweli, nawashukuru sana na wale waliojitolea vyombo mbalimbali vya usafi pamoja na magari” amesema Msigwa.

Diwani wa kata ya Kitanzini ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jescar Msambatavanu alipopigiwa simu kutolea maelezo juu ya kutoonekana katika zoezi la usafi alisema yupo msibani Njombe.

“Nipo Njombe tmsibani tangu jana nimefiwa na Bibi yangu. Sasa hivu tunajiandaa kwenda kuzika” alisema Msambatavanu.

Naye Diwani wa Kata ya Mshindo Daudi Albert alipopigiwa simu mara tatu (0754-897134) kutolea maelezo juu ya kutokuonekana kwake, simu ilipokelewa na mwanamke na ambaye alikata kujitambulisha na kusema yupo makambako.

“Huyo mtu simjui mimi nipo Makambako labda umekosema namba” alisema mwanamke huyo bila na kukata kutaja jina lake.

No comments:

Post a Comment