masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, January 23, 2013

Haki za binadamu zizingatiwe na kuheshimiwa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma akifungua semina ya waandishi wa habari wa Mkoa huo katika ukumbi wa maktaba ya Mkoa.


Washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Kuu wa Mkoa wa Iringa Christine Ishengoma pamoja na msafara wake mara baada ya kufungua mafunzo ya waandishi wa habari.


Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuwa mawakala wa elimu juu ya haki za binadamu na utawala bora ili kuiwezesha jami kujua haki na wajibu wao katika maisha ya kila siku.

Haya yamezungumzwa na Mkuu wa mkoa wa Iringa Christine Ishengoma alipokuwa akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya haki za binadamu na utawala bora yaliyofanyika leo katika ukumbi wa maktaba ya Mkoa huo.

“Kupitia mafunzo haya, muwasaidie wananchi kujua haki zao pamoja na utawala bora ili waweze kuwajibika pale wanapotakiwa kuwajibika” amesema Ishengoma.

Amessema ili jamii iweze kujua haki zao ni lazima waandishi waelimishwe vizuri kwa kuwa wao ndio wasambazaji wa elimu na taarifa kwa jamii.

“Wanahabari ni muhimu sana kwa nchi yoyote ile duniani. Hii ni kwamba mwanahabari ni chombo muhimu katika usambazaji wa elimu kwa jamii na wao ni kiungo kikubwa kati ya serikali na jamii katika mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mwana habari ni mtu wa kuheshimiwa kwa kuwa ni watu wakutegemewa” amesema.

Nance Ngula afisa uchunguzi na utawala bora ambaye alikuwa mkufunzi ameseme kila mtu anahusika katika suala zima la haki za binadamu na utawala bora kwa kuwa ndio walengwa wa masuala hayo.

Amesema ukiukwaji wa haki za binadamu unaweza kufanywa na mtu yeyote yule bila aidha kwa kutumia wadhifa alio nao au kwa makusudi na kutowajibika katika nafasi.

Ngula aliwata waandishi kuwa na utaratibu wa kuzifikia jamii na kujua changamoto wanazokabiliana nazo na kutumia nafasi walizo nazo kwa kuwasaidia kuondokana nazo aidha kwa kutumia elimu yao au kutafuta msaada mbadala.

Naye Shoma Philip afisa uchunguzi mkuu wa haki za binadamu na utawala bora alisema utawala bora ni pamoja na kuzingatia haki zote za binadamu katika ngazi zote bila kujali umri.

Amesema hata utoaji mimba ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwa unakiuka haki ya kuishi ambayo kila mtu anatakiwa kuipata.

“Utawala usiozingatia haki za binadamu hauwezi kuitwa utawala bora kwani ili haki ziweze kuzingatiwa lazima kuwepo na utawala bora” amesema.

Amesema kila wakati migogoro mingi inasababishwa na ukosefu wa utawala ulio bora kwa kuwa haki za binadamu zinakuwa hazithaminiwi.

Aidha amesema jamii pia ina wajibu wa kutimiza yale ambayo yanawapasa ili kusiwe na migongano na malalamiko kwa upande wao.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na kuratibiwa na idara ya haki za binadamu na utawala bora katika serikali.


No comments:

Post a Comment