CHAMA cha
Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa kinalalamikiwa kuwaandaa vijana kwa ajili ya
kuhujumu chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kudhoofisha harakati
za mabadliko.
Taarifa
zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa CCM imeandaa wanafunzi 200 katika Chuo
Kikuu kishiriki cha Mkwawa ili waweze kutumika katika mkutano unatarajiwa
kufanyika leo katika viwanja vya Mwembetogwa katika Manispaa ya Iringa.
Taarifa
zinasema CCM wametengeneza kadi na fulana zenye nembo ya Chadema ambapo
wanafunzi 200 wa Mkwawa wamepewa kadi hizo na shilingi 5,000/= kila mmoja ili
wajifanye kama wanachama wa Chadema ili waweze
kurudisha katika mkutano huo utakaofanywa na Philip Mangula.
Rais wa
serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa Mtama Joseph amethibitisha
kuwepo kwa taarifa hizo ndani ya chuo hicho na kusema kuwa njia inayotumika ni
watu waliopoteza mwelekeo.
“Ni kweli
kuna taarifa kama hizo zimezagaa hapa chuoni na kama unavyosema ni kweli kwamba
kwa mujibu wa taarifa ninazozikia hapa chuoni kuna wanafunzi 200 ambao
inasemekana wamepewa shilingi 5000 kila mmoja na kupewa kadi zenye nembo ya
Chadema ili warudishe kwenye mkutano wa CCM utakaofanyika kesho 26 Januari mwaka huu katika
viwanja vya Mwembetogwa” alisema.
Mtama
alisema watu walioshindwa kufikiri na kuwajibika hutumia mbinu chafu kwa kuwa
hawana fikra zingine na kwamba wanaotumia rushwa ni wale waliofeli kung’amua
wajibu wao na kufiki rushwa ndiyo njia sahihi.
“Watu
walioshindwa kung’amua mambo na kuwajibika hutumia rushwa kama
njia mbadala kwao kwa kuwa hawana kitu kingine cha kufanya. Lakini ambacho
ninaweza kusema ni kwamba watu wanapokubali kununuliwa kwa muda mfupi wafikiri
baadaye wataishije. Ila inapofika wakati wa kufanya maamuzi wawatupilie mbali
watu wanaotumia njia kama hizo ili liwe
fundisho kwao” alisema Mtama.
Awali Katibu
wa Chadema katika Manispaa ya Iringa Suzan Mgonukulima alisema kuna mbinu chafu
zilizobainika kutumika kuhujumu Chadema ambazo wananchi wanatakiwa kuwa nazo
makini.
Alisema kuna
baadhi ya watu ambao wametengeneza kadi na fulana (t-shirt) zenye nembo ya
Chadema ili kutumika katika mikutano na watu kwa kujivua uanachama wa chama cha
Chadema kwa kurudisha kadi hizo kama njia ya
kukidhoofisha chama.
Mgonukulima
alisema kutokana na hilo itakapotokea mahali
popote tendo hilo
linafanyika wananchi wanatakiwa kujua kuwa ni mchezo mchafu uliotengenezwa na
na watu.
Alisema kwa yoyote atakayefanya hivyo na kubainika kuwa anatumiwa na si
mwanachama wa chama cha Chadema atachukuliwa hatua kali za kisheria ili aweze
kueleza uanachama wake katika chama cha Chadema ulitoka wapi na kadi
aliyoirudisha ilitoka wapi na alipata kwa njia zipi.
Naye Katibu
mwenezi wa Chadema katika Wilaya ya Iringa mjini Joseph Mgima alisema kutokana
na hujuma wanazofanyiwa Chadema mara kwa mara wamekuwa wakitoa taarifa kwa
jeshi la polisi lakini kumekuwa na ukimya hali inayoonesha kupuuzwa na jeshi hilo bila sababu.
“Tumekuwa
tukihujumiwa mara kwa mara na kila tunapohujumiwa tumekuwa tukitoa taarifa kwa
jeshi la polisi lakini hakuna hatua iliyochukuliwa hadi sasa jambo linaloonesha
kusababisha uvunjifu wa amani” alisema.
Alisema
baadhi ya wanachama wamekuwa wakitumiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa
kukihujumu Chadema kwa kuahidiwa kupewa shilingi laki tano kila
wanapofanikisha.
Alisema
katika mkutano wa CCM uliofanyika katika maeneo ya Soko Kuu katika Manispaa ya
Iringa jumapili iliyopita baadhi ya wanachama waliotumika kama
wasanii kwa kuihujumu Chadema walitoboa siri hiyo.
Kwa upande
wake Kaimu Mwenyekiti wa Chadema katika Manispaa ya Iringa Charles Ndenga
alisema mbinu inayotumika kwa kuhujumu chama chake ni watu wasio na fikra ambao
wanasubiri kufa na kuzikwa kisiasa.
“Cha ajabi
ni kwamba viongozi wa CCM wanatoka katika ofisi zao wakijua kabisa ilani yao haijatekelezwa na
kufika kwa wananchi na kunadi uongo wa maneno hali wakijua kabisa wanawahadaa
wananchi na badala yake wanaamua kutengeneza mbinu chafu za kuhujumu vya
vingine vyenye hoja za msingi” alisema.
Diwani wa
Kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi (CHADEMA) ambaye pia ni mjumbe wa kamati
tendaji ya Wilaya alisema propaganda za CCM ni sawa na mtoto anayekula vumbi
bila kujua anakula kitu gani.
“Kila wakati
nazishangaa sana
propaganda za CCM kwa sababu zinafanana na mtoto anayekula vumbi bila yeye
kujua anachokula. Hizo ni dalili za mtu aliyekufa huku akitembea akisubiri
kuzikwa. CCM wanatapatapa kwa sababu wanajua kuwa mwaka 2015 wanaachia ngazi na
Chadema tunashika dola” alisema.
Katika hatu
nyingine mmoja wa vijana wanaosemekana kutumiwa na CCM kwa kukihujumu Chadema
amefunguka mbele ya gazeti hili akisema kuwa ameahidiwa shilingi laki tano
(500,000/=) na CCM pindi atakapofanikisha hujuma hiyo.
Kijana huyo
ambaye aliomba jina lake lisiandikwe kwa ajili ya usalama wake alisema tayari
kuna vijana 17 ambao wameandaliwa kwa kazi hiyo na tayari zimekwisha
kutengenezwa fulana 200 na kadi 370 na CCM zenye nembo ya Chadema ili ziweze
kutumika katika matukio mbalimbali yakiwemo ya kuanzisha fujo katika mikutano
ya Chadema ili Chadema iweze kuchafuka pamoja na kadi kutumika katika mikutano
ya CCM kawa wanachama kurudisha kadi na kujiunga na CCM.
Akifafua
zaidi alisema njia itakayotumika ili kuwachanganya wananchi, CCM wamepanga
kusomba wakulima vijijini kwa magari na kuwagawia kadi hizo walizozitengeneza
ili watumie majukwa kama kurudisha kadi kwa ajili ya kuwatumainisha wananchi kama Chadema hakifai.
“Nakuomba
ndugu mwandishi, nimekwambia hayo yote lakini usiniandike katika gazeti. Yapo
mengi lakini kama unavyoona hali ilivyo kwa
leo tuishie hapa wasije wakanishtukia. Kwa usalama wangu naomba usiniandike
jina” kilisema chanzo chetu.
Wakatika
hayo yakizungumzwa katika wa CCM Mkoa wa Iringa Emanuel Mteming’ombe alisema
katika mkutano utakaofanyika leo katika viwanja hivyo wanatarajia kupokea
wanachama wapya kati ya 400 hadi 500.
Alisema katika
mkutano huo ambao utafanywa makamu mwenyekiti wa CCM Philip Mangula, atapokewa
na wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini Iringa ambao watakuwa wateja wakubwa wa
kuingia katika chama chake.
“Baada
ya mkutano wake wa hadhara siku ya pili atakutana na viongozi wa chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Iringa kufanya tathimini ya ziara yake kabla ya kurejea
jijini Dar es Salaam,hata hivyo ziara hiii ni fupi lakini badaye atakuja
kufanya ziara katika Wilaya zote za mkoa wa Iringa”alisema.
Mtemeng’ombe
alisema miongoni mwa waanchama wanaotarajia kujiunga na CCM wengi wanatoka
katika vyuo vikuu vilivyopo mkoani hapa alivyovitaja kuwa ni Mkwawa, Tumaini,
Ruaha (RUCO) na baadhi yao
ni vijana walio katika Manispaa ya Iringa Mjini.
“Hawa
tunaowaingiza kuwa wanachama wa CCM ni wale tuliofanyia usaili kwa muda mrefu,
tumewafundisha katiba ya chama,namna ya kuishi maadidli ya chama na kanuni
tunazozitumia,sisis hatuchukua wanachama barabarani bali tunafuata taratibu
tulizojiwekea na ndio sababuwanachamwetu ni wa uhakika” alisema Mteming’ombe na
kuongeza.

No comments:
Post a Comment