masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, December 11, 2012

Waliobomolewa nyumba na mvua iliyoambatana na upepo mkali waomba msaada wa haraka.

Kulia ni Mbunge wa viti maalum Ritha Kabati asikiliza matatizo ya baadhi ya wananchi wa kijiji cha Migoli waliobomolewa nyumba zao na mvua iliyoambatana na upepo mkali.

Mbunge wa viti maalum Ritha Kabati akiongea na waathirika wa kimbunga Migoli.

Baadhi ya waathirika wa kimbunga wakimsikiliza Mbunge alipowatembelea kijijini Migoli.

Nyumba ya Rhoda Mwangosi mkazi wa kijiji cha Migoli iliyobomoka baada ya kupigwa na mvua kubwa pamoja upepo mkali.

Vipande vya mabati ya nyumba ya Rhoda Mwangosi vikilivyokusanywa nje ya jengo lililobomoka.

Ritha Kabati akiongea na nesi wa kituo cha afya cha Migoli nje ya jengo lililoezuliwa.

Moja ya nguzo za umeme ikitengenezwa baada ya kuangushwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali.


KUTOKANA na mvua kubwa zilizoambatana na upepo mkali kuvunja nyumba zaidi ya 50 pamoja na kuezua paa katika kata ya Migoli na Nyang’olo, wilaya ya Iringa na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi walioharibiwa na nyumba zao wanaomba msaada wa haraka kutoka kwa wasamalia wema.

Wananchi waliopatwa na mkasa huo walitoa kilio chao jana walipotembelewa na Mbunge wa viti maalum Ritha Kabati (CCM) aliyefika Migoli kutoa pole kwa waathilika hao.

Rhoda Mwangosi alisema hana mahali pa kuishi hadi sasa kutokana na kukosa fedha za kununulia mabati ya kuezeka.

“Mimi hapa nilipo sijui nifanye nini kwa sababu nimekosa nyumba na sina mahali pa kulala. Sina pesa za kununulia mabati kwa sababu hili suala halikutegemewa kutokea. Tunaomba wanaoguswa watusaidie kwa kweli” Mwangosi.

Steven Kabelege alisema nyumba zilianza kubomoka toka muda mrefu lakini kwa msimu huu imekuwa zaidi ya vipindi zilivyopita.

“Nyumba zilianza kubomoka tangu muda mrefu lakini ilikuwa ni nyumba moja, mbili au tatu lakini kwa kipindi hiki hali imekuwa tofauti kwani upepo umekuwa wa aina yake; umekuwa mkali kuliko kipindi cha nyuma” alisema Kabelege.

Kituo cha afya nacho kilipatwa na kasa huo baada ya kuezuliwa kwa jengo na kusababisha usumbufu kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa.

Agnete Mwinuka ambaye ni nesi wa kituo hicho alisema wakati paa linapoezuliwa kulikuwa na wagonjwa 9 ambao walikuwa wamelazwa na kutokana na mkasa huo mmoja alizidiwa.

“Wakati paa linaezuliwa kuwalikuwa na wagonjwa 9 waliokuwa wamelazwa. Mara tu mmoja alizidiwa kwa mshtuko tukajitahidi kumhudumia akapata nafuu” alisema Mwinuka.

Awali afisa Mtendaji wa Kata ya Migoli Bosco Mwiyowela akitoa taarifa kwa Mgunge huyo, alisema zaidi ya nyumba 50 zimeathilika minoni mwake zikiwemo nyumba za taasisi na mashirika mbalimbali ya kidini.
Hata hivyo wananchi walijikuta wapo gizani kutokana na nguzo za umeme udondoshwa.

Hosen Juma mfanyakazi wa shirika la umeme Tanesco alisema jumla ya nguzo 16 zilidondoshwa na mvua pamoja na upepo huo hali iliyosababisha hasara kubwa kwa wananchi wanaofanya kazi kwa kutegemea nishati hiyo hasa wafanyabiashara wa samaki, vinyozi na kituo cha afya.

Ritha Kabati alitoa unga wa sembe kilo 100 na kuahidi kutoa mchango wake kadiri atakavyoweza ili kusaidia wananchi wanaohangaika kutokana na tatizo hilo.

“Mimi nimekuja kuwaona na nijue nini hasa kinatakiwa kwa sababu sikujua nichukue nini lakini nikaona nisije mikono mitupu nikanunua kilo 100 za unga walau mpate chakula. Baada ya kusikiliza matatizo yenu na kuona hali halisi ilivyo nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu ili nitoe mchango” alisema Kabati.

No comments:

Post a Comment