masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Wednesday, December 12, 2012

MAKUHANI WAASWA

Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akihubiri katika Kanisa la Bikira Maria Consolata - Mshindo.

Mhashamu askofu Evaristo Chengula wa jimbo Katoliki la Mbeya akimuwekea mikono Shemasi Deogratias Lyimo Mtika.

Shemasi Deogratias Lyimo Mtika akiwa amelala kifudifudi wakati wa kusali litania ya watakatibu wakati wa kuwekwa daraja la upadre.

Pd. Deogratias Lyimo Mtika mara baada ya kupata daraja Takatifu la upadre.
MAKUHANI wametakiwa kudumisha heshima ya wazee kwa kufuata mongozo wa uchungaji katika kazi zao za kiroho ili waweze kuwa watumishi waaminifu katika kutekeleza kazi waliyokabidhiwa.
Haya yamezungumzwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa katika Misha ya daraja la upadre iliyofanyika leo katika Kanisa la Bikira Maria Consolata Parokia ya Mshindo katika jimbo la Iringa.
Mhashamu askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa jimbo hilo amesema kazi ya kuhani ni kuelekeza na kufundish ayaliyomema pamoja na kuwashauri waliopoteza mwelekeo wa amani kurudi katika kutenda haki.
Amesema kuhani anapoacha kazi anayotakiwa kufanya na kujiingiza katika upotoshaji ni hatari kwani huwa ni chanzo cha amani kupotea na kujipotezea imani kwa watu wanaomtegemea kimawazo na kimtazamo kwa kufuata njia iliyo sahihi.
Amesema kazi ya utume si ya mzaha na hivyo kila wakati lazima Mungu apewe nafasi ya kwanza kwa kila anachotaka kukifanya ili kiwe na baraka kwa ajili ya watu.
“Bidii ya kusali iwe mbele ili Mungu azidishe nguvu katika utendaji na kutoa maamuzi yaliyosahihi kwa ajili ya kupatanisha na kufundisha; kulegea kusali ni kukaribisha udhaifu wa mafundisho ya kweli nay a haki” amesema.
Amewataka kutoona aibu katika kukiri imani na kusimamia imani popote kwani kufifia kiimani ni kukaribisha mvurugano katika uadilifu na utumishi.
“Hubirini kwa bidii bila kuionea aibu imani yenu kwani mkilegea tu mtakuwa mmekaribisha kupotea kwa maadili yenu na utumishi wenu utakuwa ni wa mashaka” alisema.
Amesema kuwa popote wanapofanya kazi wanatakiwa kuwa na mahusiano mazuri na watu wanaowatumikia ili amani na upendo viendelee kuwepo kwa ajili ya kulijenga taifa la Mungu.
“Watumikieni watu wote bila kubagua kwa kuwa na mahusiano mazuri mkihubiri amani, upendo na mshikamano ili taifa la Mungu liendelee kuwa na upendo. Mkiwa kinyume na hayo mtatowesha amani na kusambaratisha watu kwa kuwagawa katika matabaka na makundi yasiyo na sababu” amesema.
Hata hivyo amewataka wasitawaliwe na mambo ya kidunia yaliyo kinyume na maadili ya utumishi wao ili kuendeleza heshima ya uadilifu na upendo.
“Kumbuka unapowekewa mikono na wazee, heshima yao iendelee kupitia tabia na maadili yako unapokuwa kwenye huduma. Usiwe mtu mwepesi kiasi cha kudharaulika kitabia na kiuadilifu” amesema.
Misa hiyi ilikwenda sambamba na utoaji wa daraja takatifu la upadri kwa Shemasi Deogratias Lyimo Mtika wa shirika la wamisionari wa Biokira Maria Consolata huku ikihudhuriwa na Mhashamu askofu Evaristo Chengula wa jimbo la Mbeya pamoja na viongozi mbalimbali wa dini na serikali.

No comments:

Post a Comment