masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, December 20, 2012

MKIZIMA TV NA SIMU TUTAANDAMANA: CHAHDEMA

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Peter Msigwa akiwahutubiwa wakazi wa Manispaa ya Iringa katika viwanja vya Mwembetogwa.

Mbunge wa Musoma mjini Vicent Nyerere akiwahutubia wakazi wa Manispaa ya Iringa katika viwanja vya Mwembetogwa.

Mamia ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Mbunge wa Musoma mjini Vicent Nyerere katika viwanja vya Mwembetogwa.
 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeahidi kufanya maandamano nchi nzima endapo serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) watazima simu wanazoziita feki pamoja na runinga, Januari 1, 2013 kwa sababu ya teknolojia ya digitali (Joerg: hakuna uhusiano kati ya simu na mfumo wa digitali! Irekebishwe!)

Akiongea jana Jumatano, tarehe 19 mwezi huu, katika mkutano wa chama hicho uliofanyika katika kiwanja cha Mwembetogwa, Iringa Manispaa, Mkoani Iringa Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mhe. Vincent Nyerere alisema kuwa, serikali ya Chama cha Mapinduzi inadhamiria kumkandamiza (Joerg: Nadhani ni maneno khali sana...) Mtanzania wa hali ya chini.

“Nawaambia wakizima simu na TV tutaingia barabarani. Ingekuwa mimi ndio mwenye Serikali na Msigwa na Dokta Slaa na wengine, tungefanya hivi; Marufuku kuingiza simu feki ili zilizopo zitumike mpaka zioze zenyewe, lakini sio kwa kuzima simu wa runinga bali kuwapa wananchi taarifa wasinunue simu feki“, alisema Nyerere.

Aliongeza kuwa simu hizo hazitengenezwi nchini bali hutoka nje ya nchi, lakini Serikali imeendelea kusisitiza juu ya wazo lake la kupiga marufuku simu feki, huku yenyewe ikiendelea kuziingiza nchini.

“Hizi simu hazitengenezwi hapa zinatoka nje, huingia nchini aidha kwa kupitia uwanjwa wa ndege au mpakani ambapo serikali yote ipo pale wakiwemo polisi, TRA, usalama wa taifa wapo. Hata hivi tunavyoongea kuna simu za kichina zinapitishwa kuingia Tanzania”

Aliongeza “Haiwezekani simu bado zipo sokoni, watanzania wote hawajapata habari, wanaendelea kununua na zinawasaidia halafu serikali inataka  kunazima. Ndiyo maana nikimwona mtu amevaa nguo ya CCM namshangaa sana”

Wakati huo huo CHADEMA kimeahidi kufanya jitihada ya kudai twiga waliosafirishwa nje ya nchi huku wakidai kuwa waliochukua twiga hao waadhibiwe.

“Waziri kivuli wa maliasili na utalii, tunaomba twiga wetu warudi, hatutaki fedha zao. Hatuhitaji kitu kingine zaidi ya kurudishiwa Twiga, wazungu waje na sio kuwapelekea“, alisema Nyerere.

“Waliochukua twiga waadhibiwe. Sitaki kuamini kwamba ni Maige pekeyake alijipanga, akaenda porini, akakamata twiga, akafunga, akabeba akapeleka kwenye ndege. Wote waliokwenda kufunga twiga hao, walioidhinisha, wote wachukuliwe hatua”, alisema Nyerere.


Aidha aliwataka wabunge nchini kuhakikisha ifikapo Julai 2013 Waziri Mkuu anaeleza Mwenge unatumia shilingi ngapi kutembea nchini, nani anahoji fedha hizo na bajeti yake inatoka wapi? Na kudai kuwa wanachi hawataendelea kutoa michango ambayo haitolewi takwimu juu ya kiasi kilichochangwa, matumizi na kiasi cha pesa kilizobaki.

“Taifa lilipokuwa dogo mbio za Mwenge zilikuwa ni sawa tu, lakini sasahivi miaka 50 ya Uhuru, mbio za Mwenge sasa basi. Mbio za Mwenge zipo kwasababu Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya na wengine wanapiga dili na polisi wanakaa nyuma kwenye defender wanasindikiza koroboi inawaka nchana” alisema Mbunge huyo.

Hata hivyo Nyerere alisema kuwa haoni sababuya kuwepo waziri wa viwanda wakati nchi yenyewe haina hata kiwanda kwa kuwa hiyo ni moja ya matumizi mabaya ya fedha za ewalipa kodi.

“Kuna sababu gani ya kumpa waziri asimamie viwanda wakati hatuna viwanda? Mnaongezea ukubwa wa serikali na kupoteza fedha za walipa kodi pasipo sababu yo yote” alisema.

Aidha alisemsa watu wanapokuwa na shida ya maji, viongozi wanachukua pesa za walipa kodi na kununulia magari na kuwaacha wananchi katika matatizo.

“Watu wanashida ya maji lakini tumeletewa magari kila kona ya maendeleo ya ya programau ya maji. Je, watu wanashida ya mari au wanashida ya maji?” alisema.

Alisema maendeleo siyo imani inayozungumzwa kwa maneno bali ni vitendo na utekelezaji.

“Maendeleo sio imani ambayo unasema utaeleza kwa maneno na kuwaaminisha watu. Maendeleo yanatakiwa kutekeleza kwa vitendo” alisema.

Wakati huo huo Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa alizungumzia, baadhi ya viongozi wa CCM ambao wamekuwa wakifanya ujanja wa kuwapigia simu wafuasi wa CHADEMA kwa lengo la kuwanunua, huku baadhi yao wakionesha kukubali.

“Ujanja wa CCM wanajua kabisa kama wananchi hamuwataki, njia pekee wanayotumia mpaka sasa ni ile ile ya kujaribu kuwarubuni watu, hivi ninavyozungumza pale ofini  kwangu wanachama makini wanapigiwa simu sana na viongozi wa CCM wakitaka kuwanunua huku baadhi yao wakionesha dalili za kununuliwa. Wale wanaopenda kwenda ni bora wakaenda mapema” alisema Msigwa.

No comments:

Post a Comment