| Hadija Juma mwenye umri wa miaka 105, mkazi wa Mtaa wa Fumilwa, Kata ya Mji Mpya katika Manispaa ya Morogoro akiongea na mtandao huu nyumbani kwake. |
AJUZA Hadija Juma mwenye umri wa miaka 105, mkazi wa Mtaa wa Fumilwa, Kata ya Mji Mpya katika Manispaa ya Morogoro, amemwomba, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere amsaidie kupata haki zake zilizoibwa.
Bibi huyo ambaye hajui kwamba Mwalimu Nyerere alishafariki dunia tangu Oktoba 1999, alisema anamtaka amwonee huruma na kumtembelea nyumbani kwake ili aweze kumsaidia kupata hati yake ya nyumba aliyotapeliwa na watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wajukuu wake pamoja na pesa zake anazodai kwa watu mbalimbali.
“Nimetapeliwa hati ya nyumba yangu nilipokuwa naumwa. Walikuja wajukuu wangu wawili wakasema wanakwenda kuninulia dawa kumbe walikuwa na lengo la kuniibia hati ya nyumba,” alisema na kuwataja kwa jina mojamoja (tunayo), akisema ni wakazi wa jijini
Akifafanua zaidi bibi huyo alisema wajukuu hao hawana haki ya kumiliki hati hiyo kwa kuwa si halali.
“Naomba kwa Nyerere anisaidie kupata haki yangu. Hawanipi hati yangu ya nyumba, wanataka kuniua ili nisiendelee kudai. Hata Kikwete naye naomba anitembelee anionee huruma mimi nipate haki zangu,” alisema.
Bibi huyo alisema amefikia hatua hiyo kutokana na polisi waliofikishiwa taarifa hizo kumwomba hela mara kadhaa, huku wakishirikiana na wadeni wake kuficha haki zake.
“Mimi naomba Nyerere na Kikwete wanisaidie kwa sababu suala hili nimelipeleka polisi, lakini kila wakati wanataka hela pasipo kufanya lolote. Kila wakati wanataka hela tu, sasa mimi na uzee huu nizipate wapi? Nimetoa hela nyingi, lakini hadi sasa wamenidanganya. Nyerere mzee mwenzangu njoo mimi nakufa sasa.
“Mimi sina uwezo, ningekuwa najiweza ningekwenda mwenyewe Ikulu kwa Nyerere nikamweleze na Kikwete na
Mbali ya kuwatuhumu wajukuu zake, bibi huyo amewataja watu wengine wanane (majina tunayo) anaodai wamekataa kumlipa fedha zake, jumla ya sh 6,750,000, hivyo kuishi katika maisha magumu.
Uchunguzi
wa mtandao huu, umebaini kuwa taarifa za bibi huyo na wadeni wake,
zipo ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, ambapo mdaiwa mmoja mkazi wa Dar es Salaam (jina
tunalo) ameweka dhamana ya hati ya gari kuwa dhamana ya deni lake.
No comments:
Post a Comment