masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Sunday, December 23, 2012

Chiku Abwao kuwanufaisha wanawake.

Mbunge wa viti maalum Chiku Abwao akiongea na wanakikundi cha wanawake cha Mafuruto Mlandege Manispaa ya Iringa.

Chiku Abwao akiwasikiliza wanawake wakimueleza namna watakavyofanya biashara baada ya kupata mkopo.

Chiku Abwao akiwaeleza mbinu za kufanya biashara wanakikundi cha Mafuruto.

Mbunge wa viti maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Chiku Abwao amezindua kikundi cha wanawake ili kuwawezesha kupiga hatu mbele kimaendeleo.

Akizindua kikundi cha Mafuruto kilichopo Mlandege aliwataka akina mama hao wawe waaminifu na wenye kujituma ili kuendelea mbele badala ya kurudi nyuma huku akikemea vitendo vyote vinavyoweza kukwamisha maendeleo.

Alisema ili kikundi kiwe cha kudumu, lazima kiwe na watu wenye dhamira njema na wenye kujituma na wanaouchukia umaskini.

“Nawaomba wapenzi wangu, kila mtu adhamilie kwa nia njema. Tuukatae umaskini na kuuchukia wala tusikubali kuukumbatia kwa kukatishwa tamaa na watu waliofilisika kifikra” alisema Abwao.

Amewataka wanawake hao wanapojiunga na vikundi wahakikishe kuwa wanawajulisha waume zao ili kuepusha mpishano unaoweza kujitokeza ndani ya nyumba pindi mwanamke huyo anapoonekana kupiga hatua ya kimaendeleo.

Hata hivyo alisema kila wakati maendeleo huletwa na watu wenyewe kwa kutumia nguvu za mikono yao huku akiwataka wawe mawakala wazuri wa maendeleo na kikundi kiwe mfano wa kuigwa na vikundi vingine.

“Unapoingia kwenye chama cha siasa usitegemee kupewa bila kujishughulisha. Maendeleo yako yataletwa na wewe mwenyewe kwa kutumia jitihada zako” alisema.

Kwa upande wa katibu mtendaji wa chama hicho Yusta Udamwa alisema mtu anayempa mwenzake akili humtakia mema katika maishani kuliko mtu anayegawa pesa aidha kwa ushawishi wa kutaka apewe wadhifa.

“Mtu anayekupa akili ni zaidi ya pesa kwa sababu huyo ndiye rafiki yako wa kweli. Angalia sana mtu anayekupa pesa na kukushawishi umuone ni mtu wa maana, huyo hakutakii mema maishani kwa sababu anakufanya uwe mbumbu na ombaomba” alisema Udamwa.

Udamwa aliwataka akina mama wenzake kuwa bega kwa bega na Mbunge huyo ili ili kuendelea kufaidika na mawazo ya maendeleo pamoja na kuendelea kupata masaada wa kukwamua maisha yao.

Chiku Abwao ameanza kuviinua vikundi hivyo baada ya kumaliza kutoa elimu ya ujasiliamali katika kata zote 16 za Manispaa ya Iringa ambapo alikizindua kikundhi hicho kwa shilingi 320,000/= ambazo zitaanza kukopeshwa kwa wanakikundi hicho kwa ajili ya kufanyia biashara ndogondogo.
Chiku Abwao akitoka kwenye nyumba aliyokuwa akifanyia kikao na wanakikundi.

No comments:

Post a Comment