JAMII
ya wawindaji na waokota matunda wa kabila la Wahadzabe waliopo katika Wilaya ya
Karatu mkoani Arusha ni changamoto kubwa iliyoligubika zoezi la uandikishaji wa
sensa ya watu na makazi iliyofanyika Agosti 26 baada ya jamii hiyo kutoa
masharti ya kupatiwa nyama ili wahesabiwe.
Hayo yalisema jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS), Dk. Albina Chuwa wakati wa kufunga mkutano wa tano wa baraza la
wafanyakazi wa ofisi hiyo uliofanyika kwa siku mbili mjini hapa.
“Katika
mambo ambayo tumejifunza wakati wa zoezi la kitaifa la uandikishaji wa sensa ya
watu na makazi iliyofanyika Agosti 26 mwaka huu ni wenzetu Wahadzabe namna
ambavyo walitoa masharti kwa
serikali wapatiwe nyama na wakahesabiwa. Kwa kweli ilikuwa changamoto kubwa na
tumejifunza mengi na kimsingi tunazifanyia kazi changamoto
zilizojitokeza,”Alisema Chuwa.
Jamii ya Wahadzabe haijishughulishi na kazi za kilimo wala
ufugaji na badala yake, wanategemea uwindaji na kuokota matunda kama njia kuu ya kujipatia chakula.
Desemba 31 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kutangaza matokeo ya sensa ya watu na makazi wakati atakapolihutubia taifa katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka ambapo pamoja na mambo mengine, atatangaza idadi ya watanzania waliopo nchini hivi sasa.
Desemba 31 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kutangaza matokeo ya sensa ya watu na makazi wakati atakapolihutubia taifa katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka ambapo pamoja na mambo mengine, atatangaza idadi ya watanzania waliopo nchini hivi sasa.
Sensa ya watu na makazi ilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka
1910, sensa nne za mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967,
1978, 1988 na 2002.
Hata
hivyo wakati taifa likisubiri kwa hamu kubwa taarifa hiyo ya Rais
Kikwete , Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi
ya milioni 34 kutokana na sensa ya watu na makazi iliyofanyika kwa mara ya
mwisho mwaka 2002.
Kwa
upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayoub alisema kuwa
umma unapaswa kuelimishwa kwamba matokeo yaliyopatikana katika zoezi la
uandikishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka huu yatatumika kuongeza ubora
na kupanua wigo wa uzalishaji wa takwimu za msingi kama vile pato la taifa, mfumuko
wa bei na takwimu za viashiria mbalimbali vya kijamii na kiuchumi.

No comments:
Post a Comment