masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, December 20, 2012

MICHANGO MINGI KIKWAZO KWA WATOTO YATIMA


Na Happiness Matanji, Iringa

Moja ya changamoto zinazovikabili vituo vya kulelea watoto yatima ni michango mingi katika shule za msingi pamoja na ushirikiano mdogo wa baadhi ya shule na vituo hivyo.

Akiongea katika sherehe ya chakula cha pamoja cha kuikaribisha Krismas ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Dtk Christine Ishengoma, Mkurugenzi wa kituo cha Daily Bread Life Tanzania Mkoani Iringa,Mchungaji Mpeli Mwaisumbe alisema kuwa michango hiyo ni mzigo mkubwa kwa vituo.

"Ofisi ya Elimu Manispaa au Mkoa inaagiza shule watoto hawa wasilipe michango lakini tunazo risiti na kila siku ya Mungu walimu wamekwa wakikaidi na wamekuwa wakitudai na wanatudai michango hiyo kwa namna kubwa; Michango ya ulinzi, maji, michango mingi. Rim paper inakaratasi 500 lakini kila mtoto anaambiwa akalete rim paper moja" alisema Mwaisumbe.

Alieleza changamoto nyingine kuwa ni kutokupata ruzuku kutoka Serikalini, majengo ya shule kuhitaji ukarabati, uhitaji wa chumba cha kompyuta pamoja na maktaba, lakini pia kutopata michango ya wanachama na wanachi kwa wakati na hivyo kuwa na wakati mgumu kununua mahitaji muhimu na kulipa Ankara mbvalimbali.

Hata hivyo alieleza mafanikio mbalimbali ya kituo hicho kuwa jamii imekwisha elimika na kuona wa michango yao kwa kituo hicho, kituo kimepata shamba kijiji cha Mgera kwa ajili ya kilimo na ufugaji. Kituo hicho kimeweza pia kununua Bus aina ya Coaster pamoja na treka kwaajili ya kilimo.

Kituo hicho kimeweza kuanzisha mradi wa Cherehani na pia kuongezewa kituo cha Nzi chenye watoto 23 wa kike na kiume kwaajili ya kukiendesha.

Mchungaji Mpeli alisema kuwa kutokana na changamoto ya maji katika kijiji cha Nzi, kituo kinatarajia kuchimba kisima kirefu kwaajili ya matumizi ya kituo na pia kuwasaidia wakazi wanaoishi katika kijiji hicho.

Katika sherehe hizo baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakishirikiana na kituo hicho akiwemo Geodfrey Mungai na Safina Mungai walisema kuwa, wamekuwa wakisaidia kituo hicho tangu miaka 5 iliyopita kutokana na kituo hicho kufanya kazi nzuri ya kijamii.

Sarafina Mungai alisema kuwa kunabaadhi ya vituo vimukuwa vikitumia misaada kwaajili ya maslahi yao binafsi badala ya kuwasaidia watoto.

"Kwa mtazamo wangu mi naona sisi kama binadau tunakuwa na tamaa, ile misaada tunayoipata hatuitumii vile inavyotakiwa, mtu anaona ile hewla aipeleke kwake akafanyie mambo yake badala ya kuwalewa watoto. Yani minaona tubadilishe mtazamo wetu, tuone huyu mtoto nayeye anahitaji upendo kama angekuwa na mzazi wake asingeweza kumfanyia hivyo.

Aidha kituo hicho hupokea watoto kutoka ustawi wa jamii kwa utaratibu wa sheria na maamuzi makini kati ya kituo na ustawi wa jamii na mkoa kuamua nani anastahili kuwa katika kituo baada ya uchunguzi makini.

Kituo hicho kilianza kupokea rasmi watoto mwaka 2004, mpaka sasa kituo hicho kinawatoto 58 ikiwa 35 kutoka DBL Mkimbizi na 25 kutoka kituo cha Nzi.

Hata hivyo jumla ya watoto waliopokelewa na na kituo hiki ni 51 lakini waliopo sasa ni 35 ambapo kati yao 7 walipata walezi, 21 wapo Sekondari, na 11 wapo katika shule za msingi, lakini pia kupitia shirika hilo watoto zaidi ya 150 wanapewa msaada wa vifaa vya shule nje ya kituo nchi nzima kwa msaada wa shirika la Pro Africa.

Aidha Mchungaji Mpeli amesema sherehe ya chakula cha pamoja kwaajili ya kukaribisha krismas na mwaka mpya hufanyika Desemba kila mwaka ambapo amewashukuru wadau wote ambao wamekuwa bega kwa bega katika kukisaidia kituo hicho.

No comments:

Post a Comment