| Ilula stars wakiondoka na gari baada ya kupokea zawadi ya ushindi kiwanjani hapo kurudi nymbani kwao Ilula. |
Mchezo
wa bonanza uliochezwa jana katika kiwanja cha Mahenge kata ya Mahenge
Wilaya ya Kilolo katika Mkoa wa Iringa, Ilula stars waliweza kuibuka na
ushindi katika nafasi ya mshindi wa kwanza na kujichukulia zawadi nono.
Bonanza
hiyo iliyoandaliwa na Stacom Kitonga Hotel ilishirikisha timu 8 za
vijana kwa lengo la kuinua vipaji vya vijana ambapo vinaja hao waliibuka
na zawadi mbalimbali.
Ilula
stars ilweza kuibuka na ushindi huo baada ya kuichabanga Mgowelo mabao
2-1 katika nafasi ya nusu fainali mabao yaliyofungwa na Amani Myovela na
Nansuli Mbululo yaliyopatikana katika dakika ya 16 na 22 katika kipindi
cha kwanza huku Mgowelo wakiambulia goli moja lilofungwa na Fanye
Ng’eve katika dakika ya 10 katika kipindi cha pili.
Katika
hatua hiyo ya nusu fainali, Magana na Mahenge walishindwa kuoneshana
ubabe ndani ya dakika 90 za mchezo na kulazimishana sare ya bila
kufungana hali iliyolazimika kupigwa mikwaju ya penati na kuwezesha timu
ya Mahenge kuingia katika fainali kwa mabao 6-5.
Katika
nafasi ya kutafuta mshindi wa tatu, timu ya Magana ilitolewa na Mgowelo
kwa goli 1-0 lililofungwa na Gawe Masambuli ambalo lilipatikana kwa
njia ya penati ndani ya daki za mchezo.
Timu
ya Mahenge ilishindwa kutamba mbele ya Ilula stars katika fainali baada
ya kulambwa bao 1-0 na kufanikiwa kuingia katika nafasi ya mshindi wa
pili.
Alikuwa
Salim Kaywanga wa Ilula stars aliyeipatia timu yake ushindi baada ya
kujitisha kichwani mpira wa kona iliyopigwa na William Chang’a katika
dakika ya 19 katika kipindi cha kwanza.
Katika
ushindi huo Ilula stars ikashika nafasi ya mshindi wa kwanza na
kujipatia zawadi ya pampu ya maji yenye thamani ya shilingi laki nne
(400,000), Mahenge mshindi wa pili wakijipatia zawadi ya seti ya jezi na
fadha tasilimu shilingi sabini elfu (70,000/= huku Mgowelo ikiwa
mshindi wa tatu wakijipatia fedha tasilimi shilingi laki moja na
ishirini elfu (120,000/=).
Jumla
ya timu 8 zilizoshiriki katika bonanza hilo ni Nice Moab kutoka kijiji
cha Mahenge, Mahenge Shooting Stars kutoka kijiji cha Mahenge, Home
Boy’s kutoka Ruaha Mbuyuni na Black Stars Ruaha Mbuyuni.
Timu
zingine ni Fire Store kutoka kijiji cha Msosa, Magana Sports kutoka
kijiji cha Magana, Mgowelo kutoka kijiji cha Mgowelo na Ilula Stars
kutoka Ilula.
Black
Stars waliweza kujipatia fedha tasilimu shilingi hamsini elfu
(50,000/=) kama timu bora huku mchezaji bora akiwa Juma Ismail kutoka
timu ya Magana akijipatia fedha taslimu shilingi elfu kumi (10,000/=).
Gawe
Masambuli kutoka timu ya Mgowelo alijipatia fedha taslimu shilingi elfu
kumi (10,000/= kwa kuwa mfungaji bora huku olikipa bora akiwa Shafii
Ngenzi wa timu ya Mahenge shooting stars akijipatia shilingi elfu kumi
(10,000/=) wakati huo marefalii watatu wakikijipatia ishirini (20,000/=)
kila mmoja.
Akizungumza
na mtandao huu kwa niaba ya mwandaaji wa bonanza hilo Stacom Kitonga
Hotel, Wallafrid Mgina alisema nia ya hoteli ya Kitona ni kuwaunganisha
vijana katika upenda pamoja na kujenga mahusiano mazuri baina ya hoteli
ya Kitona na wananchi.
“Sisi
tunataka kuwaunganisha vijana katika upendo na kujenga mahusiano baina
yetu na jamii ili iweze kutambua uwepo wetu na huduma tunazozitoa. Pia
tunataka kile kidogo tunachokipata tusaidiane” alisema Mgina.
Mgina
alisema pia anataka kuwakumbusha wafanyabiashara kuwa wananafasi kubwa
katika kutoa michango yao kwa jamii inayowazunguka badala ya kusubiri
kuombwa misaada tu.
“Vile
vile tunataka kuwakumbusha wafanyabiashara kuwa wakati wakat ambao
wanatakiwa kutoa ushirikiano na jamii ni pale wanapotoa sehemu yao
badala ya kusubiri kuombwa” alisema.
Bonanza
hilo limekuwa changamoto kubwa kwa viongozi mbalimbali wa serikali hasa
wanasiasa kwa pale wanapokuwa wahamasishaji wa michezo bila kuwepo na
utekelezaji.
Akizungumza
katika mahojiano na mtandao huu, diwani wa viti maalumu wa kata ya
Mahenge Sheila Ngailo alisema kuwa inabaki kuwa changamoto kwao katika
kuandaa michezo kwa vitendo.
“Hii
inabaki kuwa changamoto kwetu kwa kuwa tumekuwa wahamasishaji bila
kufanya kwa vitendo. Kazi inabaki kwetu kama viongozi wa maeneo husika”
alisema.
No comments:
Post a Comment