masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, December 6, 2012

Wasomi msitumie fikra za weninge: Askofu








Wasomi wametakiwa kutumia elimu na mawazo yao katika kukuza uchumi wa taifa badala ya kutegemea akili za wengine katika kwa fikira za kupata maendeleo.

Hayo yalisemwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa katika Mahafali ya tano ya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO).
Mhashamu askofu Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa jimbo la Iringa alisema ni hatari kubwa kwa taifa na watu wake kwa wale waliopewa dhamana kukopa fikra na mawazo kutoka sehemu nyingine bila kuwa na uwezo wa kujitegemea.

“Msiende kukopa fikra wala mawazo kutoka kwa watu wengine mkifikiri kuwa ndiyo njia sahihi ya kuleta maendeleo na kukuza uchumi kwani ni hatari kwa taifa na watu wake. Kutegemea kukopa fikra na mawazo kutoka sehemu nyingine ni kutliangamiza taifa” alisema.

Amewataka wahitimu kutumia elimu yao kuwa wazalendo wa kweli na kusimamia haki za watu na kulinda rasilimali kwa kuipenda nchi na kumpenda kila mmoja.
“Elimu yenu iwe taa ya kuleta uzalendo wa nchi katika kulinda rasilimali, kuipenda nchi pamoja na kumpenda kila mmoja” alisema.

Pia alisema elimu yao iwe kwa ajili ya watu kwa maendeleo ya watu kutetea haki, ukweli na moyo wa uwajibikaji huku akiwataka kutokuchezea elimu kwa kuangamiza maisha ya wengine.

“Elimu yenu iwe kwa ajili ya watu na maendeleo yao kwa kutetea haki zao, ukweli na ichochee moyo wa uwajibikaji. Ili nchi iweze kusonga mbele msichezee elimu yenu kwa kuangamiza maisha ya wengine” alisema.

Naye mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Mt. Agustino Tanzania Mhashamu askofu John Ndimbo alisema wasomi wasiostaarabika na kutumia fursa hizo kwa fikra za kufanya kazi katika mashirika makubwa na nchi zenye nguvu ya kiuchumi badala ya kufanya kazi kwa manufaa ya maendeleo ya nchi ni sawa na kufanya uhaini.

“Wahitimu wengi fikra zao ni kuwa na ndoto za kufanya kazi katika mashirika na nchi zenye nguvu ya kiuchumi badala ya kufanya kazi kwa manufaa ya maendeleo ya nchi. Huo ni uhaini kwetu” alisema askofu Ndimbo.

Amewataka wahitimu kuwa mawakala wa nidhamu katika nchi popote pale ili nchi iweze kurudishe heshima iliyopotea kwa sababu ya watu wasioitakia mema kuendelea kuimaliza kwa kufanya mambo ya ajabu ukiwemo wizi wa mali za taifa.
“Mkawe mawakala wa zuri wa nidhamu, kaweni chachu ya mabadiliko ya maendeleona mkawe chachu ya mabadiliko ya uadilifu. Kuelimika ni kustaarabika. Mkawe mwanga wa ustaarabu” alisema.
Wakati huo huo Waziri wa Fedha na Mipango William Mgimwa alisema maendeleo ya elimu yanakwenda sambamba na mategemeo ya wazazi, walezi na wadau wengine ambao wanawatumia wahitimu katika kazi zao kwa jamii.

Alisema kwa hatua nzuri ambayo chuo kimefikia, isiwe ni mwisho bali kiwe kivutio cha wale wenye kiu ya elimu ya juu nchini pamoja na kuwa taa inayomlika pande zote ili watu waone mema yanayoendelea kufanyika katika utoaji huduma kwa kuwa mfano mzuri katika vyuo vikuu vipatavyo 40 vilivyopo nchini.
Alisema chuo kisichozingatia utoaji huduma ulio bora, kitakuwa katika ulanguzi wa elimu hali ambayo inaweza kusababisha taifa kupata walanguzi wa elimu badala ya kupata wasomi.

Mahafali hayo yalihusisha jumla ya wahitimu 1287 ikiwa ni ongezeko la asilimia 75 ya wahitimu wa mwaka jana yaliyokuwa na umla ya wahitimu 751.

No comments:

Post a Comment