ZAIDI ya watoto 800,000 wenye umri chini ya miaka mitano nchini, hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa nimonia.
Mratibu wa huduma ya chanjo Mkoa wa Iringa, Naftal Mwalongo, alibainisha hayo mjini hapa jana katika kikao cha Kamati ya Huduma ya Afya ya Msingi kilichofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kusema kuwa vifo hivyo ni sawa na asilimia 14 ya watoto wanaoambukizwa ugonjwa huo.
Alisema ugonjwa huo huenea zaidi kutokana na uwepo wa aina ya vimelea vya Streptokokas (Streptococcus) na kusababisha magonjwa ya homa ya ini, ugonjwa wa pua na mafua, ugonjwa wa masikio na uambukizo wa bakteria kwenye damu.
Alizitaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni mgonjwa kupumua kwa shida huku akiwa na kikohozi, homa pamoja na kushindwa kula au kunyonya.
Mwalongo alisema katika Mkoa wa Iringa zaidi ya watoto 47,000 walio na umri chini ya miaka mitano wameugua ugonjwa huo katika kipindi cha mwaka jana, huku mwaka 2010 waliokumbwa na ugonjwa huo wakiwa 45,953.
Aidha, alisema tatizo lingine linalowasumbua watoto waliolazwa katika vituo vya huduma za afya ni ugonjwa wa kuhara.
Alisema idadi ya wagonjwa wa kuhara chini ya miaka mitano kwa kipindi cha mwaka 2010-2011 walikuwa 70,365 ambao walipata matibabu ya nje.
Alieleza kuwa, changamoto zinazokwamisha kufanikisha kukabiliana na tatizo la kuhara ni uhaba wa vifaa vya ubaridi vya kuhifadhia dawa za chanjo na kutokuwepo kwa umeme wa uhakika katika bohari za kuhifadhia dawa za chanjo katika halmashauri.

No comments:
Post a Comment