masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Thursday, November 29, 2012

BENKI YATAPERIWA ZAIDI YA MIL. 30

BENKI ya wananchi waishio Vijijini, Village Community Bank (VICOBA) ya mkoani Iringa, imetaperiwa zaidi ya shilingi Milioni 30 na mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni mratibu wa Vicoba ambapo  aliwachangisha wananchi fedha kwa madai ya kuwapatia mikopo.

Akitoa tarifa hizo mbele ya mchumi wa Mkoa Adam Swai, katika uzinduzi wa Vicoba Lumuli katika Wilaya ya Iringa, mratibu wa Vicoba mkoa wa Iringa Tisiana Kikoti alisema fedha hizo zilikusanywa na mwanamke (Jina limehifadhiwa) aliyejitambulisha kuwa yeye ni mratibu wa Vicoba, ambapo alikusanya zaidi ya shilingi Milionbi 30 katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

“Tumepata hasara kubwa kwani mtu huyo amechukua fedha kwa kutumia cheo changu cha uratibu, na taarifa za awali nilizipata kutoka katika kijiji cha Kitumbuka, Kata ya Ilole ambako alichukua zaidi ya shilingi Milioni 12 na point,” Alisema Tisiana.

Tisiana alisema katika Kata ya Ibumu Wilaya ya Kilolo mtu huyo pia alikusanya fedha kwa vikundi mbalimbali, kwa kutumia udanganyifu huo huo na wananchi baada ya kutoa fedha hizo ambazo alidai atawapatia mikopo alitokomea kusikojulikana.

Alisema baadhi ya wananchi bado wamekuwa wakifika katika ofisi yake ya Vicoba mkoa wakilalamikia utapeli huo, na kuwa mtu anayefanya matukio hayo si muhusika wa ofisi yake, huku akiwaasa wananchi kuacha kutoa fedha kwa watu kwani hao ni waraghai.

Aliwataka wananchi kutotoa fedha kwa watu wasio na vielelezo na uhakika kutoka katika ofisi wanazodai kufanyia kazi, kwa kuraghaiwa kupatiwa mikopo, kwani banki ya Vicoba haichukui fedha bali inatoa elimu tu kwa wanachama.

“Wananchi niwambie kuwa wawe makini na mataperi hao, kwani sisi Vicoba hatuchukui hela ya mtu yoyote, tunachofanya ni kutoa elimu tu ya kuendesha vikundi vyao vya akiba na mikopo, na waratibu wangu wote wa wilaya huwa wanabarua zinazowatambulisha,” Alisema Tisiana.

Aidha alisema kutokana na tatizo hilo wananchi wamepoteza imani juu ya vicoba na kuiomba serikali iingilie kati juu ya udanganyifu huo ikiwa pamoja na kumkamata mwanamke huyo anazunguka amaeneo mbalimbali
kunachangisha fedha na hivyo kurudisha nyuma maendeleo yao.

Mratibu wa Vicoba Wilaya ya Kilolo Christina Kawaganise alisema mwanamke huyo alianza kwa kuhamasisha uundwaji wa vikundi na kufanikiwa kupata wanachama wengi na badaye kuwaambia wanavikundi wampe hela ambazo zitakuwa ni dhamana ya kuchukua fedha benki ili awapatie mikopo.

“Wengine walitoa laki tano, laki sita hadi laki 8, na katika kikundi cha MUWAKI alichukua laki moja na nusu, ninawataka wananchi wawe makini na viongozi waanzirishi wa vikundi, wengine wanalengo la kujinufaisha wenyewe na sio kuleta maendeleo kwa wananchi, Alisema Christina.

Hata hivyo mchumi wa mkoa wa Iringa Adam Swai alisema ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Kilolo kufuatilia suala hilo, na kuna haja ya kuingilia kati ofisi ya mkoa ili kuwachukulia hatua matapeli hao kwa
lengo la kumfikisha mtu huyo katika vyombo vya dola, ikiwa  pamoja na kurudisha fedha za wananchi hao.

“Uongozi wa wilaya uwafahamu hao watu, ikishindikana mkoa utaingilia kati ili tuwachukulie hatua, lakini maofisa ushirika, maofisa maendelkeo ya jamii na mkurugenzi washirikiane kumbaini mwanamke huyo taperi,” Alisema Swai.

No comments:

Post a Comment