masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, November 26, 2012

TANESCO IRINGA YAPATA HASALA YA ZAIDI YA 70 MILIONI

SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO katika Mkoa wa Iringa limepata hasara ya zaidi ya shilingi Milioni 70, baada ya wananchi wasio waaminifu kutumia nishati hiyo pasipo kulipia na wengine kutumia kwa njia zisizo halali na kuliingizia Taifa hasara.

Hatua hiyo imebainika katika msako wa Kamata Wezi wa Umeme – KAWEU unaoendelea mkoani hapa, ambapo limefanya oparesheni katika baadhi ya nyumba mjini Iringa, Makambako na Ifunda katika Wilaya ya Iringa.

Akizungumzia hasara hiyo, meneja wa TANESCO Mkoa wa Iringa Injini Dornat Makingi alisema hasara hiyo ilitokana na baadhi ya wateja wasio waaminifu kujiunganishia umeme, huku wengine wakichepusha nyaya za wa mita ili kutumia umeme mwingi kwa malipo kidogo.

Injini Makingi alisema baadhi ya wateja wao wanawatumia mafundi wa mitaani almaarufu kama “Vishoka” ambao wamekuwa wakiwarubuni wateja ili kupata fedha kwa kazi hiyo ya uhujumu uchumi.

Aidha alisema kupitia zoezi la KAWEU tayari wamewakamata wateja wengi, ambapo wateja 17 tayari wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu mashtaka ya tuhuma zinazowakabili, na kuwataka wananchi kuacha mara moja tabia ya kuwatumia Vishoka.

“Nadhani hapa wananchi wanatakiwa wafike katika ofisi zetu za Tanesco ili kuingia makubaliano ya kurejeshewa umeme pindi wanapokatiwa, na wasiwatumie hao vishoka, kwani wanaoingia matatani ni wao wateja pindi wanapokutwa wakiiba umeme na kulisababishia hasara kubwa shirika,” lisema.

Meneja mwandamizi Tanesco nyanda za juu kusini magharibi Salome Nkondola alisema katika kukabiliana na tatizo hilo la wizi wa nishati ya umeme, wameanzish zoezi endelevu la kufanya ukaguzi wa Mita nyumba
kwa nyumba.

Nkondola alisema katika zoezi hilo wataungana kimikoa ili kuongeza nguvu ya pamoja  kuwabaini wateja wanaoiba umeme kwa kuwa watu wa aina hiyo wanalisababishia shirika na Taifa hasara kubwa ya fedha.

“Tumekuwa tukipokea taarifa kwa wananchi wenye mapenzi mema na Tanesco na hivyo kufanya zoezi hilo ili kutambua kiasi cha umeme kinachoibwa, na taarifa hizo tumefanikiwa kuwakamata wateja wengi wanaoiba nishati umeme,” Alisema.

Naye ofisa usalama wa Tanesco Renalda Ngowi alisema wananchi wengi wanawatumia mafundi wa mitaani (Vishoka) katika kuchepusha umeme, na kujiunganishia, ambapo katika zoezi hilo wamefanikiwa kuwakamata zaidi ya wateja 50, 37 kutoka Makambako na 13 wa Ifunda.

Nao wateja walisema baadhi ya watu wanaojiita mafundi kutoka Tanesco ndiyo wamekuwa wakipita mitani kutaka kufanya kazi hizo, na kuliomba shirika hilo litoe elimu kwa wananchi, ili waepukane na adha hiyo ya kukamatwa na kukatiwa umeme, kupitia makosa ya Vishoka.

Isack Mnyambwa alisema yeye ni mpangaji katika nyumba za shule, na hakuwa anafahamu kama nyumba hiyo mita yake haisomo umeme anaotumia licha ya kukaa katika nyumba hiyo kwa zaidi ya miaka miwili.

Rahma Chikota alisema tatizo hilo linatokana na wakazi kubadilishana, na hivyo wanaoingia kutotambua kama kuna wizi wa umeme ulifanyika, kwa kuwa walimu wamekuwa wakihamishwa na hivyo kushindwa kutambua aliyefanya uharibifu huo.

Aldo Muyinga alisema walijiunganishia umeme huo kutoka nyumba jirani baada ya kukatiwa kutokana na kutofahamu kama kufanya hivyo ni kosa, kwani bili walikuwa wakichangia kutoka katika nyumba ambayo ilikuwa inawapa umeme.

“Tulikuwa hatujui kama kuunganisha nyumba zaidi ya moja umeme kwa kutumia mita moja ni kosa, tungeomba tupatiwe elimu ili kuepukana na matatizo haya, kwani wengi huwa tunafanya makosa ya aina kama hii bila kufanhamu,” Alisema Muyinga

No comments:

Post a Comment