masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Monday, November 26, 2012

Kwa nini vijana wengi hukosa ajira baada ya mafunzo ya VETA?

MIONGONI mwa sababu zinazokatisha tamaa vijana kujiunga na vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) ni pamoja na wadau wa sekta ya ajira kuwakataa vijana hao pindi wamalizapo elimu yao na hivyo kundi kubwa la vijana hao kutokuwa na ajira kuwa kubwa.

Mkuu wa chuo cha ufundi stadi cha VETA Mkoa wa Iringa Lazaro Kitundu akitoa taarifa wakati wa mahafali chuoni hapo juzi alisema pamoja na uwepo wa jitihada mbalimbali za kutafuta sehemu za kufanyia mafunzo, kama ni sehemu ya vitendo kwa wanafunzi, lakini wadau wamekuwa wakikataa kuwapokea wanachuo wake.

Kitundu alisema baadhi ya wadau wamekuwa wakidai walipwe gharama za vijana hao kujifunza katika maeneo yao ya kazi na hivyo kikwazo hicho kukwamisha wanachuo hao kushindwa kupata mafunzo kwa vitendo.

“Kumekuwepo na tabia ya wadau kutowapokea vijana wetu pindi tunapohitaji wafanya mafunzo hayo, kuna vikwazo tunawekewa ikiwa pamoja na kudaiwa gharama za mafunzo yao pindi wanapopokelewa kwenye sehemu za kazi hizo", Alisema Kitundu.

Aidha alisema licha ya changamoto hiyo, pia chuo kinakabiliwa na uhaba wa mabweni, na kuwa chuo kina uwezo wa kupokea wanafunzi 350, na kati ya hao ni wanafunzi 106 pekee ndiyo wanaopokelewa kutokana na tatizo
hilo.

Alisema chuo kina nafasi za mabweni 30 ya wasichana huku ya wavulana yakiwa 76 na hivyo kusababisha idadi kubwa yawanafunzi wanaoomba nafasi za kukaa bwenini kutochukuliwa kwa kuhofia eneo la kuishi.

Honorius Honorius na Suzan Duma wahitimu wa chuo kwa niaba ya wenzao walisema changamoto kwa upande wao ni pamoja na chuo kutokuwa na vifaa vya kutosha kufundishia hasa katika Karakana ya ufundi, na hivyo mafunzo kwa vitendo kushindwa kufanikiwa kwa kiwango kizuri.

Walisema kutokuwepo kwa mitambo ya kisasa inayoendana na hali halisi ya teknolojia ya ulimwengu wa sasa, na kutokuwa na walimu wa kutosha hasa kwa masomo mtambuka ambayo yanaendana na hali ya ulimwengu ulivyo.

Pia walisema chuo kina tatizo la uhaba wa vitabu vya rejea, kutokana na mfumo wa mafunzo ya VETE kubadilika n ahivyo wakijikuta wakiendelea kusoma vitu visivyo katika wakati, hatua inatakayosababisha wengi wao kukosa ajira kwa kukosa ujuzi mpya.

Hata hivyo Meya wa miji wa Iringa Amani Mwamwindi aliwataka wahitimu hao kuendeleza ujuzi waliopatiwa ili kujifunza na kuwa na elimu zaidi katika kukabiliaana na soko la ajira linalohitaji zaidi elimu.

Mwamwindi alisema Mamlaka ya VETA bado inakazi kubwa ya kuboresha utoaji wake wa elimu kwa kusimamia, kuratibu maeneo mengine ili kuwafikia vijana wengi kwa lengo la kupunguza kiwango cha umasikini na kukuza uchumi.

Aliitaka VETA kanda iongeze idadi ya wahitimi wanaojiunga na vyuo hivyo vya ufundi kwa kuwa asilimia kubwa ya vijana wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari imeongezeka, na kuwa kuna haja kwa mamlaka hiyo pia kuongeza awamu mbili za mafunzo ikiwa pamoja na kuongeza kozi fupi.

“Ili kukabiriana na changamoto ya umasiki, VETA kanda kuna haja ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivi, kwani sasa unajua kuna idadi kubwa ya wanafunzi  wanaomaliza elimu ya msingi na Sekondari, tofauti na hapo awali, si mnajua kuna ongezeko kubwa la shele za sekondari tofauti na siku za nyuma”, Alisema Mwamwindi.

Alisema wanafunzi wa kike wajiunge na vyuo vya ufundi, ili kujikwamua katika kupata fulsa za ajira na hata kujiajiri wenyewe, na kuwataka wazazi/ walezi kuwashauri vijana wajue haki na usawa katika kupata elimu hiyo.

No comments:

Post a Comment