masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Tuesday, November 20, 2012

WAANDISHI WATAKIWA KUANDIKA HABARI YA AFYA

Mwezeshaji wa mafunzo ya uandishi wa habari za afya Dk. Ahmed Twaha akitoa mafunzo kwa waandishi
Katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard akifungua mafunyo.

Washiriki wa mafunyo wakimsikiliza mwezeshaji

WANAHABARI wametakiwa kuandika habari za afya hususani juu ya magonjwa mbalimbali na lishe, ili kuweza kuisaidia jamii kuachana na imani potofu zinazohusiana na matibabu ya magojwa

Ushauri huo ulitolewa na mtaalamu wa afya ya binadamu Dk. Ahmed Twaha muweyeshaji wa mafunzo ya uandishi wa habari za afya kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa yalizoanza jana katika ukumbi wa maktaba ya Mkoa.

Dk. Twaha alisema kuwa, habari za afza zikiandikwa mara kwa mara zitaiwezesha jamii kujua namna ya kupata matibabu kwa ugonjwa husika unaosumbua kwa wakati huo.

‘Jamii yetu inashindwa kujua nini maana ya afya kwa sababu habari nyingi haziwafikii. Hii inatokana na ninyi wanahabari kutokuandika habari za afya mara kwa mara na kusabaisha jamii iwe na imani potofu  ya kutegemea waganga wa jadi juu ya magonjwa yanayoweza kutibika hospitalini’ alisema Dk. Twaha.

Alisema habari za afya katika jamii ni za muhimu katika uimarishaji wa uchumi katika Taifa kwani nguvu kazi kubwa imekuwa ikipotea kwa sababu ya magonjwa mbalimbali ambayo yanatibika.

‘Kushuka kwa uchumi kuchangiwa kwa kiasi na kupotea kwa nguvu kazi ambayo kwa kiwango kikubwa ni magonjwa yanayotibika. Kwa hiyo kwa nguvu yenu wanahabari mnaweza kufichua magonjwa katika maeneo mbalimbali yanayoitesa jamii kwa kuamini kuwa wamelogwa badala ya kwenda kupata matibabu kwa wataalamu wa afya’ alisema.

Dk.  Twaha  alisema kutokana na  jamii kukosa  elimu  sahihi ya afya  wengi  wamekuwa  wakipoteza maisha  kwa  kukosa  msaada wa kitabibu.

 Akifungua mafunzo  hayo, Katibu mtendaji  wa IPC Frank Leonard alisema  mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo mbali mbali ambayo umoja  wa  klabu  za  waandishi  wa habari Tanzania (UTPC)  imekuwa  ikiyatoa kwa  vilabu mbalimbali nchini ikiwemo IPC.

Alisema mafunzo hayo yatasaidia ujuzi kwa wanahabari katika  kuandika habari  za afya kwa  kuzingatia ubora na taarifa sahihi katika habari zinazohusu afya.

Leonard  alisema wengi  wao  wamekuwa  wakiandika habari zinazohusu afya pasipo kuwa na utaalam na kusabababisha jamii kutokujua masuala yanayohusu afya na kutotilia maanani juu ya matibabu yake lakini kupitia mafunzo haya watakuwa na ujuzi wa kuandika habari hizo kwa undani zaidi.

Mafunzo hayo ya siku nne  yaliyoanza hapo jana ambapo yanatarajiwa kumalizika Novemba 22 mwaka huu, huku waandishi watapata fursa za kutembelea katika hospitali ya Mkoa katika vitengo mbali mbali vya afya kujua changamoto wanazokutana nazo hasa magonjwa makubwa yanayoitesa jamii.

No comments:

Post a Comment