masuguru

Tangazo la cheti

Tangazo la cheti
tangazo

KLERUU

KLERUU
KLERUU

CAPRICORN

CAPRICORN

Ibada

Ibada

Saturday, November 17, 2012

Sakata la kupigwa risasi mapadre, watu wanne mbaroni kwa tuhuma za kuhusika

Kutokana na sakata la mapadre wa Parokia ya Isimani Jimbo Katoliki la Iringa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, watu wanne mbaroni wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Hii inakuja siku moja baada ya mapare wawili wa Parokia hiyo kuvamiwa nyumbani kwao na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimba za mwili kwa silaha.

Siku moja kabla ya kuvamiwa mapadre hao watu wasiojulikana walivamia mlinzi wa Kanisa katika Parokia ya Kihesa na kumjeruhi vibaya na kitu kizito kichwani ndipo walipovunja milango ya Kanisa na kuiba pesa kadhaa, baadhi ya vyombo vya ibada na kuharibu vibaya mavazi ya ibada, vitabu na nyaraka mbalimbali kiasi cha kutotamanika tena.

Miongoni mwa vyombo vya ibada vilivyoharibiwa na watu hao ni pamoja na kuvunjwa Msalaba, Monstranti, Taberenakulo ndogo pamoja na kumwagwa ovyo Hostia Takatifu.

Usiku wa kuamkia juzi watu wanaokadiriwa kufikia saba wakiwa na bunduki, rungu na mapanga walivamia makazi ya mapadri hao majira ya saa nne za usiku, ambapo walimpiga nne Padre Angelo Burgio ambaye ni Paroko wa Parokia hiyo na kumjeruhi vibaya msaidizi wake Pd. Helman Myala fedha zaidi ya shilingi 3.9 milioni na Euro 100.

Watuhumiwa waliokamatwa kuhisiana na tukio hilo wametajwa kuwa ni Joseph Ngwale (30), Erasto Ngwale (38), Gaitan Kitwange na Anita Mwinuka wote wakazi wa Isimani.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa wananchi wa kijiji hicho mshiriki wa msako huo ambaye ametoa taarifa kwa masherti ya kutataka kuandikwa amesema walianza kupata watuhumiwa baada ya kufanya upekuzi  katika nyumba ya Josepha Ngwale na kupata goroli 37 na gram 100 huku ikipatikana silaha gobore iliyotumika katika ujambazi huo ambayo kwa usiku huo ililetwa na mwanye Joseph Ngwale ili aifiche.

Tarifa hizo zilithibitishwa na  Diwani wa Kata ya Kihorogota Costantino Kihwele ambaye alisema watuhumiwa wote wamekwisha kufikishwa polisi ili hatua za kisheria zifuate.

Hata hivyo watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na tukio la uvamizi wa Kanisa Kuu la kiaskofu Parokia ya Kihesa na kumjeruhi mlinzi pamoja na kuiba.

Kaimu wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Gwanchele Faustine amesema baada ya kumfanyia upasuaji Pd. Angelo waliweza kutoa risasi 3 sehemu ya kifuani ambazo zilikuwa zimekwama na kueleza kuwa hali zao zinaendelea kuimarika.

“Jana tulimfanyia upasuaji Pd. Angelo tukaweza kutoa risasi 3 sehemu ya kifuani ambazo zilikuwa zimekwama. Hali zao zinaendelea kuimarika huku tukifanya jitihada za kuwahudumia” amesema Dk. Faustine.

Katika hatua nyingine Dk. Faustine alisema kuwa Mlinzi wa Kanisa la Kihesa Bathlomeo Nzigilwa aliyejeruhiwa na watu hao bado hali yake ni mbaya japo kuwa kuna dalili za kuweza hata kufumbua macho.

“Mlinzi wa Kanisa la Kihesa aliyejeruhiwa na kuletwa hapa hospitalini bado hali yake ni mbaya na tumegundua kuwa alivunjika mfupa wa kichwani kwa hiyo tunaendelea kufanya utaratibu wa kuutoa. Ila kwa leo amekuwa na dalili za kufumbua macho kwa hiyo tunafanya jitihada za kumpa huduma zaidi” amesema Dk. Faustine.

Mtandao huu umeshuhudia majeruhi hao wakiendelea na matibabu huku Pd. Myala aliyekuwa akishindwa kuongea akiwa ameanza kuongea.

No comments:

Post a Comment