| Padre Angelo Burgio akiwa wodini katika hospitali ya Mkoa wa Iringa. |
| Padre Helman Myala akiwa katika hospitali ya Mkoa wa Iringa. |
Ikiwa ni siku moja tu baada ya
Kanisa Katoliki Parokia ya Kihesa Jimbo la Iringa kunajisiwa, Parokia ya
Isimani nayo imenajisiwa huku mapdre wawili wakinusurika kuuawa kwa bunduki, nondo,
marungu na mapanga usiku wa kuamkia leo na watu wasnaosadikika kuwa ni
majambazi.
Padre Angelo Burgio muitaliano wa
Parokia ya Isimani amepigwa risasi huku mwenzake Paroko msaidizi Helman Myala
akipigwa mapanga kichwani na nondo na virungu sehemu mbalimbali za mwili wake
nusura kuuawa na watu hao.
Akizungumza na waandishi wa
habari akiwa hospitali ya Mkoa, Padre Angelo Burgio Paroko anayemaliza muda
wake, alisema walitokea watu 7 majira ya saa 4:30 usiku wakavunja mageti kisha
wakaingia ndani na kuwavamia.
“Ilikuwa majira ya saa 4:30 usiku
tulipokuwa tukijiandaa kulala ndipo walipotokea watu 7 wakiwa bunduki, virungu,
nondo na mapanga wakatuvamia wakitaka tuwaoneshe pesa zilipo; wakaanza kunipiga
kwa virungu huku mmoja akiniwekea bunduki tumboni kisha wakachukua zaidi ya
milioni mbili na nusu huku mwenzangu Pd. Myala wakamchukulia shilingi milioni
moja na laki tatu (1,300,000/=) pamoja na simu zetu zote” amesema Pd. Burgio.
Hata hivyo amesema hajui mali zingine
zilizochukuliwa kwa kuwa baada ya kuvamiwa na kuumizwa hawakupata nguvu tena za
kuweza kukagua vitu vingine.
“Kwa kweli sijui uharibifu
mwingine kwa sababu baada ya kuvamiwa na kuumizwa hatukupata nguvu tena ya
kuweza kukagua vitu vingine ndipo tulipokimbizwa na wasamalia wema hospitalini”
amesema.
Kaimu wa Mganga Mkuu wa hospitali
ya Mkoa wa Iringa Gwanchele Faustine amekiri kupokea majeruhi hao majira ya saa
7 usiku.
“Tumepokea majeruhi wawili usiku
ambao ni Mapadre wa Kanisa katoliki Pd. Angelo Burgio muitaliano na Pd. Helman
Myala. Pd. Angelo amepigwa risasi upande wa kushoto na kutokea upande wa kulia
lakini kuna risasi zingine zipo kifuani tunamuandaa aingizwe kufanyiwa upasuaji
sasa hivi” amesema Faustine.
Hata hivyo alisema pamoja na
matibabu wanayoendelea kupata, hali zao zinaendelea vizuri.
Taarifa zinazolifikia gazeti hili
tunapoingia mitamboni zilieleza kuwa tayari mtu mmoja ametiwa nguvuni kwa
kusadikiwa muwa ni mmoja wa tukio hilo
la ujambazi.
Diwani wa Kata ya Kihorogota
Costantino Kihwele amesema vijana wameingia kwenye msako kila sehemu na
kufanikiwa kumkamata kijana mmoja anayesadikiwa kuwa ni mmoja wa tukio hilo akiwa na bunduki.
“kuna kijana mmoja ametiwa
nguvuni mwa vijana wa Isimani ambao waliamua kuingia msituni kufanya msako
lakini jina lake nitakwambia kadiri tutakavyokuwa
tunaendelea na msako. Usijali jina tutakutajia kwa sabu hatutaki kulitaja sasa
hivi” amesema.
Katika hatua nyingine Dkt.
Faustine amesema mlinzi wa Kanisa la Kihesa aliyejeruhiwa jana hali yake bado
ni mbaya.
“Mlinzi wa Kanisa la Kihesa
aliyejeruhiwa na kufikishwa hapa bado hali yake ni mbaya na bado tunaendelea
kumhudumia” amesema.
No comments:
Post a Comment